‘Vigogo walikuwa wanamwaga mamilioni wakati wa uhakiki wa vyeti’

0
926

Ramadhan Hassan -Dododma

KATIBU Mkuu wa Baraza la Mitihani Nchini, (NACTE) Dk. Charles Msonde, ameeleza magumu aliyopitia wakati wa kuhakiki vyeti vya watumishi wa umma, akisema baadhi ya vigogo waliotoa ahadi za fedha na wengine magari kutaka kuhonga watumishi wa baraza hilo.

Dk Msonde  alisema hayo jana jijini hapa  katika kikao cha dharura cha  Baraza la Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kilicho lenha kujadili uadilifu usimamizi wa mitihani, maslahi ya walimu, madeni ya walimu na walimu ambao wanapandishwa madaraja bila kulipwa.

 “Sasa niwaambie yaliyonipata, zoezi halikuwa rahisi lilikuwa gumu na lilihitaji moyo mgumu, nakumbuka pale Baraza la Mitihani kuna watu walikuja na maburungutu ya fedha, wakaja kuwajaribu wafanyakazi, kuna mwingine alikuwa anatoa fedha kama mnada akamkuta mtendaji mmoja kamwambia nitakupa milioni tano.

“Alivyoona anakataa akasema anampa 10 alipokataa akasema anampa 15 alipokataa akaondoka, akaona huyu mjinga, akamtafuta mwingine akamtangazia dau la milioni 20 lakini ikashindikana, wengine walikuja na funguo za magari kuwakabidhi watendaji wangu, ilishindikana kwa sababu ni waadilifu.

“Tunapata shida sana kwenye udanganyifu, kunapokuwa na changamoto mtu wa kwanza kabisa ni mwalimu asiye mwadilifu kwa sababu mwalimu akisema no (hapana) hakuna ambaye atabadilisha.

“Nikupongeze Katibu Mkuu (Seif Deus) kwa kauli yako ambayo inastahili kupongezwa, nilisikiliza nikasema hivi ndio yenye, ile ya kuwataka walimu kuwa waadilifu katika kusimamia mitihani,”alisema Dk Msonde.

Watumishi 15,00 vyeti feki

Katika hatua nyingine Dk Msonde alisema katika watumishi 512,777 waliohakikiwa vyeti vyao, 15,811 wamekutwa na vyeti vya kughushi ambapo miongoni mwao walimu pia wamo.

“Tulipewa kazi kubwa ya kuhakiki, tulifanya kwa niaba yenu, kazi tunayofanya ni kwa niaba ya walimu nchini na ilikuwa ngumu na ugumu wake wale walioghushi sio ajabu walisaidiwa kughushi na watu wengine.

“Nilipotangaza uhakiki wa mara ya kwanza tulikutana na changamoto kubwa, wengi walikata rufaa tulipoanza kuangalia hao waliokata rufaa tukagundua wameleta vyeti vipya sio vile vya awali, walivyoleta vina division  one na two lakini awamu hii wameleta cheti cha division four lakini sio kile cha mwanzo.

“Katika zoezi la uhakiki hatukutaka mtumishi atuletee, tulitaka mwajiri ndio atuletee na mkata rufaa analeta cheti cha division four ungekuwa wewe ndio upo kule kwenye sekretariet ungefanyaje?

“Mimi niliwaambia wenzangu wala tusihangaike ukiona cheti sio kile kilichowasilishwa mwanzo wala usihangaike, andika mrufani amewasilisha cheti kilichotofauti na mwajiri wake, ameghushi kwa hiyo wote tukasema wameghushi,”alisema.

Alisema baraza limejitahidi kuboresha mifumo ambayo inatengenezwa na wafanyakazi wa baraza hilo kwa kuwa ya kisasa hadi kufikia baadhi ya nchi kujifunza nchini jinsi wanavyoiendesha.

Kwa upande wake, Rais wa CWT, Deus Seif alisema sasa hivi kuna mabadiliko kwa walimu katika zoezi la kusimamia mitihani kwani wamekuwa wazalendo na waadilifu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here