26.9 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Vigogo TRL wapata dhamana

trla+bosNa Kulwa Mzee, Dar es Salaam

VIGOGO wa Shirika la Reli Tanzania (TRL), wanaotuhumiwa kuingiza nchini mabehewa 25 ya kokoto ambayo hayana vigezo wametimiza masharti ya dhamana na sasa wako nje.

Washtakiwa hao, walikuwa rumande tangu mwishoni mwa wiki baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.

Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Dar es Salaam,  Emilius Mchauru alitoa masharti ya dhamana kuwa kila mshtakiwa anatakiwa kusaini dhamana ya maandishi ya Sh milioni 10 na kuwa na wadhamini watatu kutoka serikalini au taasisi zinazotambuliwa ambapo kila mmoja atatia saini kiasi hicho cha dhamana.

Pia, washtakiwa waliotimiza masharti ya dhamana hawataruhusiwa kutoka nje ya Mkoa wa Dar es Salaam, bila ya kibali cha mahakama.

Washtakiwa wote walitimiza masharti ya dhamana, isipokuwa Mkuu wa Michoro wa TRL, Joseph Syaizyagi ambaye hajatimiza masharti.

Washtakiwa  katika kesi hiyo, ni Mkurugenzi Mtendaji, Kipallo Kisamfu, Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa shirika hilo, Jasper Kisiraga, Mhandisi Mkuu wa Mitambo, Ngosomwile Ngosomwiles. Mhandisi Mkuu, Mathias Massae, Kaimu Mhandisi Mkuu, Muungano Kaupunda.
Wengine ni Mhandisi Mkuu Paschal Mfikiri, Mhandisi wa Karakana, Kedmon Mapunda, Kaimu Mhandisi wa Mawasiliano, Felix Kashaigili, Mkuu wa Usafirishaji wa Reli, Lowland Simtengu,  Mkuu wa Michoro, Joseph Syaizyagi na  Kaimu Meneja Mkuu wa Usafirishaji, Charles Ndenge.Watuhumiwa hao wanakabiliwa na mashtaka tisa ya matumizi mabaya ya madaraka na kutumia nyaraka za uongo kwa nia ya kumdanganya mwajiri.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles