22.8 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

Vigogo Ofisi ya Waziri kortini kwa wizi

LAW1

Na PATRICIA KIMELEMETA, Dar es Salaam

MAOFISA Ugavi wanne wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Kitengo cha Maafa), wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam  kwa madai ya kuiba mali za ofisi hiyo zenye thamani ya Sh milioni 100.

Wakisomewa hati ya mashtaka mbele ya Hakimu, Respicius Mwijage, Wakili wa Serikali, Jackson Chidunda aliwataja washtakiwa hao, kuwa ni Ahmed Yusuph(48) Ofisa ugavi, Martine Tyeah(31) Ofisa Ugavi Msaidizi, Mwahija Kimata(55),Ofisa ugavi msaidizi na Halima Mwanjiro(33) Ofisa Ugavi.

Alidai  washtakiwa hao, wanadaiwa kati ya Aprili, 2014  na Septemba, mwaka huo huo katika eneo la Keko lililopo karibu na Ofisi ya Bohari Kuu ya Madawa(MSD), Temeke jijini Dar es Salaam, wakiwa waajiriwa wa Ofisi ya Waziri Mkuu, wanadaiwa  kuiba mabati 5074,Sufuria 200 na mikeka 348 vyenye thamani ya Sh 100,164,000.

Alidai  mali hizo zinamilikiwana Ofisi ya Waziri Mkuu Kitengo cha Maafa  ambazo zilitolewa kwa ajili ya maafa kupitia kitengo hicho, lakini washtakiwa hao wanadaiwa kuchukua kinyume cha sheria.

Alidai upelelezi wa shauri hilo,bado haujakamilika na kuiomba mahakama hiyo kupanga tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.

Hata hivyo, Hakimu Mwijage aliwataka kila mmoja kuwa na mdhamini mmoja ambaye atasaini bondi ya Sh milioni 25 ambapo washtakiwa hao walikidhi mashart hayo na kuachiliwa kwa dhamana.

Shauri hilo, limeahirishwa hadi Agosti 22, litakapotajwa tena.

Wakati huo huo, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imempandisha kizimbani raia wa China, Senxin Van baada ya kubainika kufanya kazi kinyume na kibali chake.

Akisomewa hati ya mashtaka mbele ya Hakimu Huruma Shahidi, Wakili wa Serikali, Novatus Mlay alidai mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo mnamo Julai, 12, mwaka huu katika kampuni ya uwekezaji ya Tenglong iliyopo Kinondoni jijini Dar es Salaam ambapo aliajiriwa kama daktari wakati kibali chake kinamruhusu kufanya kazi katika kampuni ya kutengeneza viatu ya Tong Xing kama Mkurugenzi.

Katika utetezi wake, mshtakiwa huyo aliiomba mahakama hiyo kumsamehe kwa sababu ni babu mwenye wajukuu na mlevi wa familia na kwamba katika kampuni hiyo ni Mkurugenzi ambay ameajiri watanzania wengi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles