30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Vigogo DRC wapinga vikwazo vya Marekani

KINSHASA, DRC

HATUA ya Marekani ya kuwawekea vikwazo vya usafiri maofisa wakuu wa Tume Huru ya Uchaguzi (CENI) pamoja na viongozi wengine nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) imezua hisia mbalimbali.

Serikali ya Marekani ilichukua hatua hiyo mwishoni mwa wiki kwa madai kwamba viongozi hao walijipatia utajiri kwa njia za rushwa.

Msemaji wa CENI, Jean Pierre Kalamba, kupitia barua iliyotiwa saini na tume hiyo, amekanusha tuhuma hizo na kuongeza kuwa ilifanya kazi nzuri kuhakikisha uchaguzi huo unafanyika kwa amani.

Kalamba ameahidi kutoa ripoti ya maandalizi ya uchaguzi kuanzia mwaka 2013 hadi ulipohitimishwa mwaka huu.

Kwa upande wake, Lambert Mende ambaye alikuwa msemaji wa Serikali ya Joseph Kabila, alisema vikwazo hivyo havitakuwa na mafanikio yoyote.

“Marekani inasimama na watu wa DRC kufuatia historia waliyoweka kufanikisha mchakato wa viongozi kupokezana madaraka kwa amani. Uchaguzi ulionesha ari ya Wakongo ya kutaka mabadiliko ya Serikali na taasisi zinazowajibika.

“Hata hivyo, kuna madai hapakuwa na uwazi katika mchakato wa uchaguzi. Na kuna maofisa walionufaika na ufisadi au kuwazuia watu kuandamana na kuwanyima uhuru wa kujieleza,” ilisema taarifa iliyotolewa na Marekani.

Viongozi waliowekewa vikwazo ni pamoja na Mwenyekiti wa CENI, Corneille Nangaa na naibu wake Norbert Basengezi Katintima.

Wengine ni mshauri wa mkuu wa CENI Marcellin Mukolo Basengezi, Kiongozi wa Bunge la Taifa, Aubin Minaku Ndjalandjoko na Rais wa Mahakama ya Katiba, Benoit Lwamba Bindu.

Marekani pia imewawekea vikwazo vya usafiri maofisa wa kijeshi na wa Serikali wanaoaminika kuhusika na ukiukwaji wa haki za binadamu na kuhujumu mchakato wa uchaguzi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles