23.1 C
Dar es Salaam
Monday, September 25, 2023

Contact us: [email protected]

Vigogo CUF waanguka ubunge

Rajab-Mohamed-Mbarouk-2MOHAMED HABIB  MNYAA-MBUNGE MKANYAGENI.masoudNa Mwandishi Wetu, Zanzibar
MATOKEO ya awali ya kura za maoni kwa wanachama wa Chama cha Wananchi (CUF) wanaowania Ubunge na Uwakilishi yameanza kutoka huku majina mapya yakichomoza kwa kupata ushindi dhidi ya wabunge wanaotetea nafasi zao.
Kwa mujibu wa matokeo ya awali yaliyopatikana mjini Unguja jana, Mbunge wa Gando, Khalifa Suleiman Khalifa (CUF), amebwagwa katika kura za maoni kwa kupata kura 81 dhidi ya Othman Omar Haji ambaye alipata kura 95 na Suleiman Salim Shukuru akiambulia kura saba.
Mbunge wa Ole, Rajab Mbaruk Mohamed, amebwagwa wakati Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) akiangushwa na Sulemain Khalifan Saidi kwa tofauti ya kura mbili.
Mbunge wa Mkanyageni, Habib Mohamed Mnyaa, ameangushwa na Khamis Mohamed Khamis huku Mbunge wa Konde Hatib Said Haji akitetea nafasi yake kwa kupata kura 300 dhidi ya Mbunge aliyepita, Dk. Ally Tarab ambaye alipata kura 42 na Bakia Juma kura Saba.
“Wabunge wengine walioshindwa katika kura za maoni ni Mbunge wa Mtambile, Masoud Abdallah Salim na Mbunge wa Magogoni Kombo, Khamis Kombo huku katika jimbo la Wawi aliyeshinda ni Waziri wa zamani wa SMZ, Juma Hamad Omari, ambaye alikuwa Waziri wa Utamaduni na Utalii wa Serikali ya Ali Hassan Mwinyi na kada wa CCM kwa wakati huo,” alisema mtoa habari wetu.
Kwa mujibu wa mapendekezo hayo, majina matatu yalipendekezwa kupigiwa kura ya maoni ngazi ya jimbo na wilaya kwa wagombea wa nafasi za viti maalumu kupata mgombea mmoja kabla ya kufanyika Uchaguzi Mkuu Oktoba 25 wa mwaka huu.
Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi wa CUF, Omar Ali Shehe alisema wanachama 517 walijitokeza kuwania ubunge, wakati 242 wanataka uwakilishi na 67 ni viti maalumu. Waandishi wa habari wanne walipenya katika hatua ya kwanza ya mchujo wa kutafuta wagombea.
Matokeo ya awali na kura za wagombea kwenye kwenye mabano zinaonyesha kama ifuatavyo;
Jimbo Kojani aliyeshinda ni Hamad Salim Maalim (198), Salim Yussuf Mohamed (57) na Haji Mussa Haji (54).
Uwakilishi katika jimbo hilo ni Salim Bakar Salim (128), Hassan Hamad Omar (113) na Hamadi Mussa Rashid (7).
Jimbo la Nungwi, Uwakilishi aliyepita ni Hassan Jani (144),
Haji Mwadini (75) huku katika jimbo la Gando, Mbunge wa sasa Khalifa Suleiman Khalifa (CUF) amebwagwa katika kura za maoni kwa kupata kura 81 huku Othuman Omar Haji akipata kura 95 na Suleiman Salim Shukuru akiambulia kura 7. Katika nafasi ya Uwakilishi,
Said Ali Mbarouk (105), Ali Yusuf (50) na Kassim Hamad akiambualia patupu.
Jimbo la Magogoni, ubunge aliyeshinda ni Saleh Mohamed Saleh (48), Salum Mussa Haji (18) na Hamadi Ali Hamadi (37), huku Uwakilishi, Ali Hamad Ali (31), Rashid Hassan Rashid (13) na Maharouk Abdallah Suleiman (9).

Matokeo hayo ya awali yanaoyesha kuwa katika Jimbo la Mpendae, aliyeshinda kura za maoni ubunge ni Omar Mohamed Omar (23), Suleiman Khamis Ali (19) na Fakih Abdallah Pandu (9).
Jimbo la Chake chake, Uwakilishi, Omar Ali Shehe (106),
Ali Bakari (97) na Mohamed Subeit (27) huku jimbo la Nungwi, ubunge, Yussuf Haji Khamis (129), Juma Nyange Omar (68) na Vuai Ame Omar (31).
Kwa jimbo la Wete Mbarouk Salim Ali (131), Seif Saleh Hamad (60) na Mwandini Abbas Jecha (30). Jimbo la Konde Hatibu Said Haji (296), Dk. Ally Tarab (42) na Bakia Juma (7).
Jimbo la Mji Mkongwe, mbunge wa sasa, Muhammad Ibrahim Sanya (57), Mohamed Nur (29) na mwanahabari mkongwe visiwani na mtangazi wa BBC, Ali Saleh ‘Alberto’ (21).
Pia mkutano Mkuu wa jimbo hilo ulipga kura ya Ndiyo na Hapana baada ya mgombea wa nafasi ya Uwakilishi, Ismail Jussa Ladhu kukosa mpinzani.
Kura zilizompigia Ndiyo ni 79, zilizompigia Hapana ni 25 na nne ziliharibika.
Alipotafuwa, Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CUF, Salim Biman, alisema hivi sasa wanaendelea kukusanya matokeo yote kwa mujibu wa utaratibu na yakikamilika itatolewa taarifa rasmi.
Kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi za CUF za jinsi ya kuwapata wagombea, atua inayofuata ni kwa Baraza Kuu la Uongozi la chama hicho ambacho ni chombo cha juu, kufanya uteuzi wa mwisho na kuamua nani atakuwa mgombea wake katika uchaguzi mkuu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,718FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles