26.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Vigogo 40 Takukuru wapanguliwa

Mwandishi Wetu-Dar es Salaam

*Wamo wakurugenzi, wakuu wa kanda

HATIMAYE  Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Diwani Athuman ameanza kutekeleza agizo la Rais Dk. John Magufuli la kuifumua na kuisuka upya taaasisi hiyo

Taasisi hiyo imefanya mabadiliko ya watumishi 40, wakiwamo wakurugenzi, wakurugenzi wa kanda, wakuu wa Takukuru wa mikoa, wakuu wa vitengo na sehemu ya makao makuu.

Rais Magufuli alitoa agizo hilo, baada ya kumwapisha Diwani Ikulu Dar es  Salaam Septemba 18, mwaka jana na kusisitiza kuwa watendaji wote wanaojihusisha na rushwa waondolewe mara moja.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya  Dar es Salaam jana na Ofisa Uhusiano wa taasisi hiyo, Doreen Kapwani ilisema uhamisho huo umehusisha watumishi hao kwenda idara nyingine za Serikali.

Taarifa hiyo, iliwataja wakurugenzi waliohamishwa, kuwa  ni Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Alex Mfungo, Mkurugenzi wa Upelelezi, Mbengwa Kasomambuto na aliyekuwa Mkurugenzi wa Elimu kwa Umma, Ekwabi Mujungu

“Taarifa hii inatolewa kutokana na  maswali yaliyowasilishwa kwetu kutoka vyanzo mbalimbali kuhusu uhamisho huu.

“Tunapenda kusisitiza uhamisho huu ni wa kawaida kama ambavyo mmekuwa mkisikia unafanyika katika wizara au idara nyingine za Serikali.

“Yawezekana kwa TAKUKURU, ikawa ni mara ya kwanza kuhamishwa kwa idadi kubwa, lakini kama mnavyofahamu, sisi kama watumishi wa umma hatulazimiki kufanya kazi katika taasisi moja tu,”ilisema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo, imewasihi wananchi kuendelee kutoa ushirikiano kwa taasisi hiyo, ikiwa ni pamoja na kutoa  taarifa kupitia simu ya dharura nambari 113 ambayo hupigwa bure.

AGIZO LA JPM

Septemba 12, mwaka jana, Rais Dk.Magufuli alimtaka Athumani kufumua muundo wa taasisi hiyo ili watendaji wanaojihusisha na rushwa wachukuliwe hatua.

Alitoa kauli hiyo jana baada ya kumwapisha CP Athumani kuwa mkurugenzi mkuu wa taasisi, ikiwa ni siku chache tangu atengue uteuzi wa Valentino Mlowola aliyekuwa bosi wa taasisi hiyo.

Rais Dk. Magufuli, alisema sababu ya uamuzi wake kumwondoa Mlowola ni pamoja na taasisi hiyo kutoshughulikia vitendo vya rushwa mkoani Mara.

“Nimekwenda pale Musoma mtu amenunua Musoma Hotel kwa miaka kumi hashughuliki, anapewa kazi za kandarasi hamalizi. Waziri Mkuu alipita hapa Mara akatoa maagizo kwa Takukuru kwamba washughulikie.

“Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Mara alilishughulikia na akamaliza tangu mwezi wa nne na akapeleka faili makao makuu, lakini hadi leo mwezi wa tisa makao makuu bado hawajalishughulikia,” alisema.

Alisema makao makuu kulikalia faili hilo ndiyo sababu iliyomfanya aone Mlowola akae pembeni akafanye kazi nyingine.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles