25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Vifo vya watoto Kagera vyapungua kutoka 812 hadi 410

Na Nyemo Malecela-Kagera

KATI ya Januari hadi Septemba mwaka huu, mkoani Kagera vifo vya wajawazito vilivyotokea ni 36 na watoto 410 ikilinganishwa na mwaka jana ambapo wajawazito waliofariki walikuwa ni 65 na watoto 812.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Marco Mbata, alisema vifo vya watoto hao ni kuanzia wale waliozaliwa wakiwa wamefariki na na waliofariki wakiwa chini ya miaka mitano.

“Idadi hiyo imepungua baada ya Kamati ya Afya ya Mkoa kugundua sababu zinazosababisha vifo hivyo na kuchukua tahadhari ikiwa ni pamoja na kutoa elimu stahiki kwa jamii ili wajawazito waanze liniki mapema na endapo kuna dalili hatarishi zipatwe ufumbuzi mapema,” alisema.

Mbata alizitaja sababu zinazopelekea vifo vya wajawazito kuwa ni kutokwa na damu nyingi kabla na wakati wa kujifungua, maralia wakati wa ujauzito, kifafa cha mimba na uzazi pingamizi wakati kwa upande wa watoto vinasababishwa na maralia, homa, vichomi na sumu za bakiteria.

Alisema kwa mwaka jana Serikali imejenga zahanati kila kijiji, kituo cha afya kila kata ambazo zinatoa huduma ya upasuaji kwa wajawazito ili wasioweza kufika katika hospital za wilaya wapate huduma stahiki.

Aliwashauri wakazi wa Mkoa wa Kagera kuhakikisha wanapata bima ya afya ya CHF iliyoboreshwa ili iwasaidie kupunguza gharama za vipimo na matibabu.

“Kila mjamzito anatakiwa kuanza kliniki wiki moja tu baada ya kupata ujauzito, itasidia kugundua viashiria vya hatari ili aambiwe nini cha kufanya kama atatakiwa kuzalia kituo cha afya au hospitali na namna ya kujiandaa kwa ajili ya kujifungua na vyakula anavyotakiwa kula ili mtoto azaliwe mwenye afya,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles