25 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 8, 2021

Vifo vya vichanga vyapungua Tanga

Amina Omari, Tanga

Maboresho ya sekta ya Afya katika Mkoa wa Tanga yamesaidia kupunguza vifo vya watoto wachanga kutoka 233 mwaka 2018 hadi kufikia 132 mwaka 2019.

Hayo yamesemwa na Mratibu wa Afya ya mama na mtoto mkoani Tanga, Dorothy Lema wakati akitoa tathimini ya hali ya huduma ya mama na mtoto mkoani humo.

Amesema kuwa upungufu wa vifo hivyo unatokana na muamko wa wazazi  kupata huduma za Afya .

“Licha ya vifo kupungua lakini bado wahudumu wa Afya wana jukumu la kuhakikisha watoto wote walioko chini ya umri wa miaka mitano wanapata huduma za Afya kwa wakati Kama mwongozo unavyoelekeza,” amesema Lema.

Aidha amesema kuwa bado kumekuwepo na changamoto ya vifo vya wajawazito ambavyo vimeongezeka kutoka 54 mwaka 2018 hadi kufikia vifo 57 mwaka 2019.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
168,540FollowersFollow
527,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles