23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Vifo vya uzazi vyapungua Rufiji

image

NA MWANDISHI WETU, RUFIJI

ZAIDI ya wakazi 5,000 wa vijiji sita vya Kata ya Mohoro  wilayani Rufiji Mkoa wa Pwani, wameweza  kupunguza vifo vinavyotokana na uzazi kupitia Mradi wa Elimu kuhusu Afya ya Uzazi na Mtoto.

Mafanikio hayo yamepatikana  katika   mwaka mmoja kupitia Taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation kwa kushirikiana na Taasisi ya Uzazi na Malezi Bora (Umati).

Takwimu hizo zilitolewa jana na Ofisa wa Programu wa mradi huo wilayani hapa, Radhia Mamboleo.

Alisema mradi huo umehusisha vijiji vya Shela, Mohoro Mashariki, Mohoro Magharibi, Ndundutawa, King’ong’o na Kwaijia.

Radhia alisema mradi huo umeleta mafanikio makubwa  ikiwamo kupunguza vifo vya mama  na mtoto, wanawake kupata mwamko wa kuhudhuria kliniki kwa wakati muafaka kipindi cha ujauzito   na kuboreshwa kwa huduma za uzazi  katika vijiji hivyo.

“Mradi umefanikiwa kupunguza maambukizi ya  a Ukimwi   na kuwapatia wanawake chanjo kwa wakati tofauti na awali.

“Lakini pia mradi huu umefanikiwa kutoa elimu kwa watoa huduma jumuishi (Waja) ambao walipatiwa mafunzo kwa ajili ya kuelimisha jamii jambo ambalo limeongeza uelewa wa masuala ya afya ya mama na mtoto katika jamii ya watu wa Rufiji,” alisema.

Kuhusu changamoto za mradi huo ambao unafikia tamati Oktoba mwaka huu, Radhia alisema kikwazo kikubwa ni maeneo ambayo ufikaji wake ni wa kusuasua.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles