27.2 C
Dar es Salaam
Monday, March 20, 2023

Contact us: [email protected]

Vifo vya dharura Tanga kupungua kwa asilimia 50

Mwandishi Wetu-Tanga


WAKAZI wa Tanga wataanza kupata huduma za dharura na za wagonjwa mahututi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga – Bombo, zinazotarajiwa kupunguza vifo vya dharura kwa asilimia 50.
Huduma hizo zimefunguliwa rasmi jana na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, wakati wa ziara yake ya siku mbili mkoani Tanga.

 Ummy alisema sasa wananchi wa Tanga hawatalazimika kupewa rufaa kufuata huduma hizo hospitali ya Muhimbili, Dar es Salaam ama KCMC mkoani Kilimanjaro.
“Serikali inaendelea kuboresha huduma za afya katika hospitali za mikoa kwa kujenga jengo la huduma za dharura lililogharimu Sh milioni 211.6 na jengo la kuwahudumia wagonjwa mahututi kwa Sh milioni 350 katika kipindi cha mwaka 2018/19,” alisema Ummy.


Alisema huduma hizo zitatatua changamoto zilizokuwepo katika hospitali hiyo na katika kipindi cha mwaka 2018/19, Serikali iliipatia Sh milioni 200 kwa ujenzi wa mtambo wa kutengeneza oksijeni.
Ummy alisema huduma hizo zinatarajiwa kupunguza vifo vitokanavyo na dharura kwa asilimia 50, huku akiongeza kuwa Serikali inatarajia kuhakikisha kuwa dawa zinapatikana kwa asilimia 100 hospitalini hapo.

Pamoja na hayo, Ummy aliishukuru taasisi ya Abbott chini ya makamu wake wa rais, Andy Wilson kwa kusaidia ukarabati wa jengo la huduma za dharura.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
210,784FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles