30 C
Dar es Salaam
Saturday, December 4, 2021

Vifo vya corona vyazidi 2,000 kwa siku moja Marekani

NEW YORK, MAREKANI

MAREKANI imekua nchi ya kwanza duniani kurekodi zaidi ya vifo 2000 vya virusi vya corona kwa siku moja.

Takwimu kutoka Chuo Kikuu Johns Hopkins zinaonyesha kuwa watu 2,108 wamekufa katika kipindi cha saa 24, huku kukiwa sasa na zaidi ya watu nusu milioni walioambukia virusi hivyo nchini humo.

Marekani hivi karibuni inaweza kuipita Italia kwa idadi zaidi ya vifo vinavyotokana na virusi hivyo kote duniani.

Lakini Mtaalamu wa Ikulu ya White House kuhusu Covid-19 anasema mlipuko unaanza kuwa wa kiwango cha chini kote nchini Marekani.

Dokta Deborah Birx, anasema kuwa kuna ishara nzuri za kupungua kwa mlipuko, lakini akaonya kuwa: “Licha ya kwamba matokeo yanaweza kutia moyo, hatujafikia kilele cha maambukizi.”

Rais Donald Trump pia amesema anatarajia Marekani kushuhudia kiwango cha chini cha vifo kuliko makadirio ya awali ya vifo 100,000 , akiongeza kuwa : 

Donald Trump

” Tunaona ishara za wazi kwamba mikakati yetu mizuri inanusuru maisha ya watu wasiohesabika “.

Rais Donald Trump pia amesema kuwa anatarajia Marekani kushuhudia kiwango cha chini cha vifo kuliko makadirio ya awali ya vifo 100,000.

Marekani sasa ina takribani vifo 18,693 na idadi ya visa vilivyothibitishwa ni 500,399, kwa mujibu wa Chuo Kikuu cha Johns Hopkins, ambacho ndicho kinachofuatilia takwimu za ugonjwa huo kote duniani.

Takriban nusu ya vifo hivyo vilirekodiwa katika eneo la New York.

Italia imeripoti vifo 18,849 huku vifo zaidi ya 102,000 vikiripotiwa kote duniani kutokana na virusi vya corona.

Watafiti walikua wamekadiria idadi ya vifo nchini Marekani ingefikia kilele chake Ijumaa na hatimae kuanza kushuka, vilishuka hadi kufikia vifo vipatavyo 970 kwa siku ilipofika Mei Mosi-siku ambayo utawala wa Trump ulikua umeitaja kama siku ya kuanza shughuli zake za kiuchumi.

“Ninataka shughuli za uchumi zifunguliwe mapema iwezekanavyo ,” Trump alisema katika hotuba yake ya siku ya Ijumaa Kuu aliyoitoa Ikulu. 

“Ninaweza kusema bila shaka ni uamuzi mkubwa ambao nimewahi kuufanya”

Hatahivyo, hakuna hatua ambayo itachukuliwa hadi serikali itakapofahamu kuwa “nchi itakua katika hali nzuri ya afya “, alisema. 

“Hatutaki kurudi nyuma na kuanza tena kupambana na virusi .”

JINSI CORONA ILIVYOBADILI MAISHA NEWYORK

Virusi vya corona vimebadili kila kitu kuhusu maisha jijini New York, na sasa imegeuka kuwa uwanja wa vifo.

Wakazi wa New York wamekua wakishitushwa na magari ya Ambulance yanayopita mara kwa mara, malori yanayobeba miili ya watu na idadi kubwa ya vifo.

Wakazi wa New York wameshitushwa na kushuhudia: magari ya kubebea wagonjwa karibu wakati wote yakiwasha vimulimuli katika mitaa iliyokimbiwa na watu.

Mara kadhaa wamekuwa wakishuhudia miili iliyowekwa kwenye mabegi ya plasitiki inayowekwa kwenye malori ya friji nje ya hospitali na sasa makaburi mapya yanachimbwa katika kisiwa Hart kwa ajili ya uwezekano wa kufanya mazishi ya pamoja.

Makaburi yaliyoko mbali , yanayoweza kufikiwa kwa njia ya maboti, ni sehemu inayofahamika kihistoria kama eneo la huzuni kwasababu ni mahala pa makaburi ya jumla yasiyojengwa na mawe kutokana na kwamba ni eneo inapozikwa miili isiyo na wenyewe.

Hifadhi ya maiti ya jiji la New York ilikuwa na uwezo wa kupokea miili mingi kabla dharura ya mazishi ya wahanga wa mlipuko wa Covid-19. Lakini sasa lazima wazikwe haraka ili kuepusha maambukizi.

Wakurugenzi wa mazishi wanaongea wazi jinsi ongozeko la vifo vinavyotisha na kufadhaisha. 

Hata kabla ya rekodi ya wiki hii ya idadi ya vifo, baadhi ya familia zililazimika kusubiri kwa wiki moja au zaidi kuizika au kuiteketeza miili ya wapendwa wao.

MATUMAINI MLIPUKO KUANZA KUPUNGUA HIVI KARIBUNI 

Dk. Anthony Fauci, Mkuu wa magonjwa ya maambukizi nchini Marekani

Dk. Anthony Fauci, Mkuu wa magonjwa ya maambukizi nchini Marekani, alisema kuwa nchi hiyo itaanza  kushuhudia kupungua kwa visa na vifo. 

Lakini akaongeza kuwa ni muhimu juhudi za kupunguza maambukizi kama kuepuka watu kukaribiana zikaendelezwa.

Ubashiri mpya wa Taasisi ya hesabu na tathmini katika Chuo kikuuu cha Washington unatabiri kuwa kutakua na vifo 60,000 ifikapo Agosti 4 kama sheria zilizowekwa zitaendelea kuwepo. 

Mwezi uliopita, Dk Fauci alikadiria kuwa kutakua na vifo walau 100,000.

Ijumaa , Gavana wa New York, Andrew Cuomo alisema kuwa data za hivi karibuni zinaonyesha kuwa jimbo limefanikiwa “kupunguza usaambaaji wa virusi “, lakini pia akaonya kuwa ni mapema mno kwa watu kuanza kupuuza hatua ya watu kutokaribiana . 

“Ingawa ni jambo linalosumbua, hata kama ni vigumu, lazima tuizoee.”

Katika hotuba yake Ijumaa Rais Trump alisema pia kuwa aliona picha za ndege zisizokua na rubani za masanduku mengi ya maiti yakiwa yamekwama kwenye makaburi ya jumla katika kisiwa cha New York cha Hart. 

Maofisa huko wanasema kisiwa, ambacho kimekuwa kikitumiwa kuzika maiti za watu wasiokua na ndugu kwa miaka zaidi ya 150, sasa wanazika miili mara tano zaidi ya kiwango cha kawaida.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,968FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles