24.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, May 30, 2023

Contact us: [email protected]

VIFO VITOKANAVYO NA UZAZI ULIMWENGUNI VYAPUNGUA

Veronica Romwald, Dar es Salaam

Vifo vitokanavyo na uzazi ulimwengu vimeripotiwa kupungua kwa asilimia 44 ulimwenguni, tangu mikakati ya kupunguza vifo ilipoanza 1990 -2015.

Aidha, kumekuwa na mafanikio makubwa katika kupunguza vifo vya watoto chini ya umri wa miaka mitano licha ya kuwapo kwa changamoto nyingi zinazohitaji kupewa kipaumbele ili kufikia Malengo Endelevu ya Dunia (SDG’s).

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Masuala ya Idadi ya Watu Duniani (UNFPA), Warren Bright katika taarifa yake aliyoituma kwa vyombo vya habari kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani yanayofanyika Mei 5, kila mwaka.

“Hapa Tanzania, UNFPA huwa tunaadhimisha siku hii, kwa kushirikiana na Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto, Chama cha Wakunga Tanzania (TAMA) na wadau wengine wa afya ya mama na mtoto,” amesema.

Amesema maadhimisho ya mwaka huu yatafanyika mkoani wa Morogoro ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu.

Amesema kauli mbiu ya mwaka huu ni Mkunga ni kiongozi katika utoaji wa huduma bora kwa mama na mtoto.

“Madhumuni ya maadhimisho haya ni kutoa hamasa kwa watunga sera na watoa maamuzi ili kuhakikisha kwamba rasilimali muhimu zinakuwepo kwa ajili ya wakunga lakini pia kutambua nafasi ya pekee waliyo nayo wakunga wenye taaluma katika Jamii,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,203FollowersFollow
567,000SubscribersSubscribe

Latest Articles