Aveline Kitomary, Dar es Salaam
Majeruhi wa ajali ya lori la mafuta mkoani Morogoro waliokuwa wakipatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), wamebaki 11 baada ya wawili kufariki dunia na kufanya idadi ya waliopoteza maisha kufikia 104. Majeruhi sita wako ICU na watano wako wodi ya Sewahaji.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumapili Septemba 1, Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano ya Umma MNH, Aminieli Aligaesha amesema waliofariki dunia ni Asha Ally (28) na Avelina Pastory (30).
“Majeruhi waliokuwa wanapatiwa matibabu wamepoteza maisha wawili ambao ni Asha Ally na Avelina Pastory sasa tumebakiwa na majeruhi 11 kati ya 47 walioletwa ambapo 36 tayari wameshapoteza maisha,”amesema Aligaesha.
Majeruhi wa ajali hiyo iliyotokea Agosti 10 mwaka huu katika eneo la Msamvu mkoani Morogoro wamebaki 11 ambapo watano wako ICU na sita wako wodi ya Sewahaji.