Vifaa Yanga kupishana U/Ndege Dar

0
1338

Na THERESIA GASPER-DAR ES SALAAM

WACHEZAJI wapya wa Yanga wa kimataifa wanatarajia kuanza kuingia leo kwa maandalizi ya msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara pamoja na  Ligi ya Mabingwa Afrika.

Yanga imethibitisha kufanya usajili mzuri  wa wachezaji  wa kigeni ambao ni  Lamine Moro (Ghana), Mustapha Selemani (Burundi), , Sadney Ukhob (Namibia), Issa Bigirimana (Burundi), Patrick Sibomana (Rwanda), Juma Balinya (Uganda) Faruk Shikhalo (Kenya) na Maybin Kalengo (Zambia).

Wakati wanzawa wakiwa Ally Ally (KMC), Abdulazizi Makame (Zanzibar) na Balama Mapinduzi (Allience) Ally Mtoni ‘Sonso’ (Lipuli FC.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Mratibu wa klabu hiyo, Hafidhi Salehe, alisema wachezaji hao baada ya kuwasili ndio wataanza kupanga programu ya mazoezi kujiandaa na msimu mpya ikiwa pamoja na michuano ya kimataifa.

“Maybin ataingia saa saba usiku wa kuamkia leo, lakini wale wengine ambao wanatoka Burundi nao wataingia leo mchana(jana), wazawa wao wataanza muda wowote kuanzia sasa kwa sababu wenyewe hawapo mbali,” alisema.

Klabu hiyo tayari imeshatangaza kufunga usajili kwa wachezaji ambao walikuwa wakiwahitaji katika msimu ujao kutokana na mapendekezo ya kocha  Mwinyi Zahera.

Yanga imepania kurudisha makali yao katika Ligi na kuchukua ubingwa ambao unaoshikiliwa na  Simba mara  ya pili mfululizo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here