23.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 28, 2021

Vifaa vya ujenzi kuuzwa kwa njia ya mtandao kuepuka mikusanyiko

AVELINE KITOMARY, DAR ES SALAAM

Meneja Mauzo wa Kampuni ya Uuzaji wa Vifaa vya Ujenzi FMJ Hardware Limited, Fredrick Sanga amesema kampuni hiyo inataraji kufanya mauzo kwa njia ya mtandao lengo likiwa ni kuepuka mikusanyiko katika kipindi hiki cha mlipuko wa virusi vya Corona.

Akizungumza leo jijini Dar es salaam Sanga amesema kuwa mnada huo utafanyika moja kwa moja  kwa njia ya mtandao siku ya jumamosi kupitia vyombo vya habari vya mitandaoni.

“Vifaa vitakavyouzwa ni aina zote za vitu vitumikavyo katika ujenzi kuanzia msingi wa jengo hadi kumaliza ujenzi isipokuwa tofali, mchanga na kokoto tu,”amesema Sanga.

Amesema kupitia mnada huo wananchi wanaweza kuagiza bidhaa wanazohitaji na kupelekewa waliopo.

“Tunamwezesha mwananchi aweze kufikia ndoto yake ya kumiliki nyumba kwa gharama nafuu na kutumia bidhaa zenye ubora.

“Hivyo wananchi wote wanakaribishwa kuufuatilia mnada huo na kununua vifaa vya ujenzi kwa kupiga simu na hata njia ya whatapp 0653312438 au namba 0716902995 lakini pia waweza kuwasiliana nasi kwa Facebook FMJ Hardware na Instagram,” amesema Sanga.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
158,460FollowersFollow
519,000SubscribersSubscribe

Latest Articles