22.3 C
Dar es Salaam
Saturday, July 13, 2024

Contact us: [email protected]

Vielelezo vya kurekodi kesi ya kina Mbowe vyapokewa mahakamani

NA KULWA MZEE-DAR ES SALAAM

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam imepokea kamera na tape recorder mbili zilizotumika kupiga picha na kuweka kumbukumbu ya sauti katika maandamano yaliyofanywa na wafuasi wa Chadema katika kesi inayomkabili Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe na wenzake.

Uamuzi wa kupokea kielelezo hicho ulitolewa jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, baada ya kupitia hoja za mawakili wa utetezi waliokuwa wakipinga kupokewa.

Kielelezo hicho kilitolewa na shahidi wa sita katika kesi hiyo, Koplo Charles.

Alidai saa 10 alasiri watu walianza kukusanyika katika Uwanja wa Buibui na mshereheshaji alitangaza kwamba viongozi wakuu wa chama wameshafika na baada ya muda wabunge na viongozi wakuu walipanda jukwaani na alimsikia Mbowe akitoa kauli za kufanya hamasa ya kuichukia Serikali.

Koplo Charles aliomba kutoa vifaa hivyo kama kielelezo, upande wa utetezi walipinga, lakini katika uamuzi wa mahakama vielelezo hivyo vimepokewa.

Hakimu Simba alisema ushahidi wa shahidi wa tisa umekidhi vigezo kwa mujibu wa Sheria namba 18 ya Elektroniki inayoweka vigezo vya kupokewa kwa vielelezo hivyo.

Awali wakili wa utetezi, Peter Kibatala, alipinga kupokewa kwa kielelezo hicho kwa madai kwamba ushahidi wa kielektroniki hauwezi kupokewa mahakamani hadi kuwepo kiapo mahususi.

Mbali ya Mbowe, washtakiwa wengine ni Mbunge wa Bunda, Ester Bulaya, Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko, Katibu Mkuu, Vicent Mashinji, Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa, Naibu Katibu Mkuu Taifa – Zanzibar, Salimu Mwalimu, Mbunge wa Kibamba, John Mnyika, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee na Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche.

Katika kesi ya msingi, washtakiwa hao wanadaiwa kuwa kati ya Februari Mosi na 16, mwaka huu wakiwa Kinondoni, Dar es Salaam kwa pamoja walikula njama na wengine ambao hawapo mahakamani ya kutenda kosa la jinai, ikiwamo kuendelea na mkusanyiko isivyo halali na kusababisha chuki na uchochezi wa uasi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles