23.9 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

Vieira amtaka Arsene Wenger kufanya usajili

VieiraNEW YORK, MAREKANI

BAADA ya klabu ya Arsenal kuanza vibaya katika michuano ya Ligi Kuu nchini England, nyota wa zamani wa klabu hiyo, Patrick Vieira, amedai klabu hiyo haiwezi kuchukua ubingwa kwa wachezaji waliopo, lazima kocha Arsene Wenger afanye usajili.

Kutokana na hali hiyo, Vieira ambaye kwa sasa ni kocha wa klabu ya Ligi Kuu nchini Marekani, New York FC, amedai kwamba klabu hiyo imekosa wachezaji ambao wamekamilika na wenye kupambana kwa ajili ya taji.
Amedai kwamba wakati mchezaji huyo anakipiga katika klabu hiyo, alikuwa na wachezaji ambao wana uwezo mkubwa na umoja kwa ajili ya kuipigania timu, hivyo kwa sasa kocha huyo anatakiwa kufanya usajili kwa ajili ya kuleta ushindani.

Nyota huyo alijiunga na klabu hiyo mwaka 1995 hadi 2005, hivyo alifanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England mara tatu pamoja na Kombe la FA mara nne. Lakini nyota huyo amedai kwamba Arsenal kwa sasa ni klabu laini, hivyo ni ngumu kutwaa ubingwa.

“Kwa sasa kila nikiangalia klabu ya Arsenal, ni kweli kwamba inacheza vizuri, lakini ninaamini kuna kitu wanakikosa hasa wachezaji ambao wamekamilika kwa ajili ya kupambana.

“Kwa hali hiyo ni kwamba, timu haiwezi kuchukua ubingwa au kushindana na klabu nyingine ambazo zimefanya usajili wa nguvu na zina wachezaji wenye kupambana.

“Tangu ligi imeanza Arsenal imecheza michezo miwili, imetoa sare mchezo mmoja na kufungwa mmoja, hii ni dalili mbaya, lakini wanaweza kubadilika kama wachezaji watatambua hilo na kocha atafanya usajili wa nguvu,” alisema.

Hata hivyo, nyota huyo anaamini kuwa klabu hiyo inaweza kukaa sawa na kufanya vizuri katika michezo yake ijayo.
Michezo mitano inayokuja kwa klabu hiyo ni dhidi ya Watford ambao utapigwa Agosti 27, huku mchezo unaofuata ni Septemba 10 dhidi ya Southampton, Septemba 17 dhidi ya Hull City, Septemba 24 dhidi ya Chelsea pamoja na Oktoba 2 dhidi ya Burnley.

Baadhi ya mashabiki wa klabu hiyo wameshindwa kuzuia hisia zao na kuanza kumzomea kocha huyo katika michezo hiyo miwili iliyopigwa tangu kufunguliwa kwa pazia la Ligi Kuu, wakidai kwamba timu hiyo haifanyi vizuri.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles