22.2 C
Dar es Salaam
Monday, October 18, 2021

VIDEO YAMPONZA MSANDO, AJIUZULU ACT

Na ASHA BANI-DODOMA


MSHAURI Mkuu wa Chama cha ACT–Wazalendo Wakili Albert Msando, amejiuzulu wadhifa huo kutokana video iliyorekodiwa huku akiwa na mmoja wa wasanii wa kike ambayo ilisambaa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii.

Katika taarifa ya chama hicho iliyosainiwa na Kiongozi wa chama hicho,  Zitto Kabwe alithibitisha kupokea kwa barua ya Wakili Msando ambapo pamoja na mambo mengine aliomba kujiuzulu wadhifa wake.

Zitto alisema Msando anawajibika  kujiuzulu kwani anapaswa kuishi kama mfano kwa jamii inayomzunguka.

 “Msando amekuwa kiongozi mwenye mchango mkubwa katika chama katika nafasi mbalimbali alizoshika ndani ya chama. Chama kinamshukuru kwa moyo wake wa kizalendo na mchango alioutoa katika chama ka kipindi chote hicho na matumaini yetu ataendelea kushirikiana nasi katika ujenzi wa chama kwa kadri atakavyoweza na atakapohitajika kama mwanachama,’’ alisema Zitto.

Alisema akiwa kiongozi wa chama hicho amemkubalia kuwajibika kwake na kumtakia kheri katika kujisahihisha kwake.

Awali Msando aliandika barua katika chama hicho huku akieleza kuwa uamuzi wake huo ni kutimiza hitaji lake la kuishi kama mfano kwa jamii inayomzunguka.

“Ni wajibu wangu kwa chama changu na nchi yangu kuwajibika kama kiongozi nitaendelea kuwa mwanachama mtiifu  nikishirikiana na chama changu katika kuhakikisha nchi yetu inaendelea mbele,’’alieleza Msando katika barua yake.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
162,220FollowersFollow
521,000SubscribersSubscribe

Latest Articles