29.8 C
Dar es Salaam
Sunday, September 15, 2024

Contact us: [email protected]

Video bora Bongo Fleva kuwa balozi wa Ziff

Ally Kiba
Ally Kiba

NA FESTO POLEA, ZANZIBAR

KATI ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya saba kutoka Dar es Salaam na watatu kutoka Uganda ambao video zao zinashindanishwa kupata moja yenye mpangilio mzuri wa hadithi za filamu, atakuwa balozi wa Ziff kwa mwaka huu.

Mkurugenzi wa Tamasha la 19 la Kimataifa la Filamu Nchi za Jahazi (Ziff), Profesa Mhando, alisema kwamba wamepanga kumpata balozi mmoja wa tamasha hilo kutokana na video za wasanii hao watakaowashindanisha ili kuleta hamasa ya ukuaji wa video za muziki nchini.

“Video itakayochaguliwa kuwa bora na majaji wetu, tutamtangaza  msanii wa video hiyo kuwa balozi wetu, tutakuwa tukimlipa kwa mwaka mzima na atatunga na kurekodi wimbo wa Ziff kwa tamasha lijalo,” alisema Profesa Mhando.

Alisema video hizo zilipatikana baada ya kutangaza kupokea video watakazozishindanisha wasanii wa muziki.

“Tulitangaza walete kazi zao na wachache wameshaleta  na atakayeshinda ndiye tunatarajia awe balozi wetu na kuleta hamasa kwa wasanii wengine kuleta kazi zao kwa tamasha la mwakani ambalo litakuwa maalumu kwa kuwa linatimiza kuwa tamasha la 20,” alisema.

Baadhi ya video zitakazoshindanishwa ni pamoja na ‘Aje’ wa Ali Kiba, ‘Sweet sweet’ wa Chege Chigunda, ‘Zigo Remix’ wa Ay aliomshirikisha Diamond Platnumz na ‘Sizonje’ wa Mrisho Mpoto.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles