29.3 C
Dar es Salaam
Saturday, May 28, 2022

Vicky Kamatta: Mwanamke ni jeshi kubwa awezeshwe

Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Vicky Kamatta akihutubia wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya ujasiriamali kwa wajane na wasiojiweza mkoani Geita

 

Na Mwandishi Wetu

MBUNGE wa Viti Maalumu (CCM), Vicky Kamatta amesema mwanamke ni jeshi kubwa ambapo ukimwezesha mmoja umewezesha jeshi kubwa lililopo nyuma ikiwamo familia na wategemezi wake.

Vicky alisema hayo wakati akizindua mafunzo ya ujasiriamali kwa wajane na wasiojiweza mkoani Geita yaliyotolewa na Asasi ya kusaidia wajane na wasiojiweza mkoani humo, Victoria Foundation inayomilikiwa na Mbunge huyo.

Mafunzo hayo yalitolewa kwa lengo la kupunguza pengo la elimu ya masuala ya fedha kwa wanawake hao kwa kuwafundisha mbinu mbalimbali za biashara, namna ya kuweka akiba na kulipa mikopo.

“Victoria Foundation mbali na kutoa misaada mbalimbali kwa walemavu, kwa sasa umeanza kusaidia elimu kwa wanawake na kuwawezesha mitaji ili waweze kufikia malengo,” alisema.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mafunzo hayo, Mkuu wa mkoa wa Geita, Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga alimpongeza Kamata kwa jitihada zake kwa kuinua wanawake hususani wajane na wasiojiweza kiuchumi na kuwataka wanawake kujenga utamaduni wa kufuatilia taarifa mbalimbali kuhusiana na masuala ya fursa za kibiashara ili kuzitumia katika kupanua wigo wa shughuli zao.

“Wanawake wengi nchini wanashindwa kusonga mbele kibiashara kwa kuwa wanakosa taarifa ambazo zingetumiwa kuwawezesha kusonga mbele na kujikwamua kiuchumi, ni wakati wao sasa kutafuta taarifa zitakazoinua biashara, mafunzo kama haya mmeyapata bure myatumie vema kuhakikisha mnatimiza malengo yenu,” alisema.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
192,631FollowersFollow
542,000SubscribersSubscribe

Latest Articles