VICHWA VYA TRENI KUSOMBA VIGOGO

0
600

Na Mwandishi Wetu,

VICHWA 15 vya treni vilivyoingizwa nchini  kupitia Bandari ya Dar es Salaam na Shirika la Reli Tanzania (TRL) kuvikana, huenda vikasababisha vigogo wa shirika hilo la reli na  wale wa Wizara ya Uchukuzi na Mawasiliano wakaingia matatani.

Walio kwenye hatari ya kukumbwa na sakata hilo ni pamoja na waliohudumu kwenye nafasi mbalimbali ndani ya  TRL na wizara hiyo tangu 2013 ambapo mikataba mbalimbali ya ununuzi wa mabahewa na vichwa vya treni iliingiwa.

Juzi Rais Dk. John Magufuli, akizungumza kwenye Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA), alisema kuna vichwa vya mabehewa vilivyoshushwa havina wenyewe.

“Vichwa 15…wamefanya mission yao na havihitajiki TRL, wanasema hawajaagiza wala hakuna document (nyaraka) yoyote waliyosaini ya kusema wanahitaji lakini vimekuja vikateremshwa hapa wala hamuulizi vimetoka wapi.

“Walivyomaliza kuteremsha TPA ndiyo mkaanza kuuliza wakati meli ilishaondoka na vichwa venyewe inasemekana ni vibovu. Ni lazima hapa kulikuwa kuna mchezo na inawezekana rushwa ilikuwa inatembea.

“Nina uhakika wizara mtakaa, inawezekanaje vichwa vinatereshwa bila kujua vinaenda wapi. “Siku nyingine watateremsha hata vifaru na mkavipokea bila kuuliza vinaenda wapi au kontena la sumu ni kwa sababu hakuna ‘coordination’ nzuri.

“Sijui TPA na wizara mtayafanyia nini labda mtayasaga yawe maskrepa. Najua hili hamtaki watu wajue sasa mimi nalisema hadharani ili Watanzania wajue na ubovu wa hapa,”alisema.

Rais Dk. Magufuli alivitaka vyombo vya dola kuchunguza inakuwaje vitu viteremshwe bila mkataba.

Baada ya maelezo hayo ya Rais, kauli ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Deusdedit Kakoko, ilivihusisha vichwa hivyo na TRL, jambo ambalo linawaweka shakani vigogo wa wizara hiyo.

Kwa mujibu wa Kakoko , vichwa hivyo vya mabehewa vilitengenezwa siku zilizopita na vingine vikatangulia na kuanza kutumika lakini mchakato wa ununuzi ulikuwa na walakini.

Alisema baadaye Serikali haikupenda kuendelea na awamu ya pili ya vichwa 11 vilivyokuwa vimebakia lakini Kampuni ya Khomaz ya Afrika Kusini ilikuwa imeshamaliza kutengeneza.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here