28.6 C
Dar es Salaam
Saturday, January 28, 2023

Contact us: [email protected]

VIBOKO HAVIMFUNZI MTOTO

NA AZIZA MASOUD,

KUMEKUWA na tabia kwa baadhi ya wazazi kutumia nguvu kubwa kuwaelekeza watoto wanapokosea.

Kila mzazi ana njia zake ambazo anaziona sahihi za kumwelimisha ama kumwelewesha mtoto wake anapokosea kulingana na historia na taratibu alizojiwekea.

Wapo wazazi ambao hawaamini katika maongezi ya kawaida yenye busara ambayo yanaweza yakampa mtoto njia sahihi ama kumbadilisha anapokuwa anafanya makosa madogomadogo, wengine wanaamua kutumia viboko wakifikiri kwamba ni njia sahihi ya kumuonya mtoto.

Wazazi wengi wanadhani mtoto ukimchapa viboko anakuwa msikivu na mtiifu, mawazo ambayo si sawa, kwakuwa viboko vinaweza vikachangia mtoto kuwa na kiburi zaidi ya alivyokuwa awali.

Viboko pamoja na kuhesabiwa kama sehemu ya adhabu, lakini havishauriwi kutumika mara kwa mara, hasa kwa watoto ambao wanafanya makosa kwa nadra kwa sababu vinaweza vikamfanya mtoto kuharibikiwa na kuwa sugu endapo utakuwa unampiga mara kwa mara.

Mtoto anapokosea unapaswa kuongea naye kwa utaratibu katika mahali sahihi, yaani nyumbani, kama mzazi unapaswa ukimsisitiza kitendo alichokifanya si sahihi na unapaswa kumwelewesha ili asifanye kitu hicho tena, anapaswa afuate njia fulani kuepuka kufanya makosa kwa wakati mwingine.

Unapompa mbadala wa kosa lake hiyo inamsaidia kuona kwamba kitu alichokifanya hakipo sahihi na kwamba asione anakosolewa bila sababu.

Wapo watoto ambao hawawaogopi wazazi wao wanapowaonya kwa maneno wakikosea, hilo si tatizo, waweza tafuta njia nyingine ya kumrekebisha  kwa kutompa vitu anavyovipenda  kwa wakati.

Mfano, mtoto anaweza kukosea ukaamua kumpa adhabu ambayo haitamuumiza, adhabu ambayo ni sehemu  ya kumjenga.

Unapaswa kumpa adhabu ndogo ndogo zitakazomtesa  kisaikolojia, mfano mtoto ni mpenzi wa kwenda kucheza  mpira na wenzake nje, kwa siku hiyo unaweza kumzuia, hiyo nayo ni moja ya adhabu, kwa hiyo unaweza kumzuia  huku ukimsisitiza kosa alilofanya ndiyo chanzo cha wewe kuchukua hatua hiyo.

Njia nyingine unayoweza kutumia pia unaweza kumnyima huduma anazozipenda ambazo si muhimu, bila kugusa suala la vifaa vya shule, mfano kama mwanao anapenda kuvaa saa ya mkononi unaweza kukataa kumnunulia kwa kipindi hicho ili ajue kama amekosea.

Kwa mzazi anayejitambua na kumwelewa mtoto wake, kiboko kinapaswa kuwa adhabu ya mwisho kabisa kwa mtoto baada ya kujiridhisha kuwa adhabu ndogondogo unazompa hazimsaidii kubadilika anapokosea.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles