24.4 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

Vibaka waiba koki za maji stendi ya mabasi

NA OSCAR ASSENGA,TANGA.

WATU wanaodhaniwa kuwa vibaka,wametumia fursa ya uwapo wa ugonjwa wa corona kuiba koki zilizowekwa kwenye ndoo za maji stendi ya mabasi madogo ya Ngamiani jijini Tanga na  kusababisha kukosekana huduma ya wananchi kunawa mikono.

Hayo yalibainishwa jana na msimamizi wa magari madogo maarufu daladala kwenye stendi hiyo, Ally Kibaya wakati wa ziara ya Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Thobias Mwilapwa alipokwenda kuangalia utekelezaji wa maagizo ya wataalamu wa afya namna ya kuchukua hatua za kukabiliana na tahadhari za ugonjwa huo.

Koki hizo na ndoo zilitolewa na Chama cha Wamiliki wa Mabasi Madogo (Taremia)  na Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (TABOA)  kuona namna ya kupambana na ugonjwa wa Corona.

Vyama hivyo viliweka ndoo hizo kwa lengo la kuwasaidia abiria kwa kuweka  ndoo za kutosha na kutafuta fundi wa kuweka koki.

Alisema  hali hiyo imewapa wakati mgumu kwa sababu  kumesababisha maji kushindwa kukaa kwenye ndoo.

Mwilapwa alisema wizi huo, ni hujuma dhidi ya mapambano dhidi ya ugonjwa  huo, ambapo alionya tabia hiyo na kiwataka wanaohusika kutokurudia na vitendo vya namna hiyo.

Alisema katika vita dhidi ya mapambano ya ugonjwa huo,hakuna sababu ya kufanya hujuma hasa kwa vile vitu ambavyo vinatolewa na watu kwa ajili ya kukabiliana na janga hili ambapo alisema kitendo hicho hakina tofauti na laana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles