28.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, June 6, 2023

Contact us: [email protected]

VETA yatakiwa kuangalia fursa za uwekezaji Vyuo vya Uvuvi nchini

Na Christina Gauluhanga, Mtanzania Digital

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako ameuagiza uongozi wa Chuo cha Mafunzo na Ufundi Stadi (VETA) kuangalia fursa za uwekezaji vyuo vya uvuvi na usindikaji samaki kwenye mikoa mbalimbali inayojishughulisha na shughuli hizo.

Wito huo ameutoa jana wakati wa makabidhiano ya vifaa vya mafunzo ya uvuvi na uchakataji samaki vyenye thamani ya Sh milioni 350 vilivyotolewa kwa Wilaya ya Chato na Serikali ya Jamhuri ua Watu wa China.

Amesema wakati sasa umefika kwa Veta kufanya urasimishaju wa vyuo hivyo kulingana na mazingira ili kuendeleza jamii na kukuza uchumi wa nchi.

Amesema wanashukuru China kwa msaada huo na urafiki wao utakuwa wa kudumu ambapo msaada huo utatumika kutoa elimu kwa jamii ya watu wa Chato kwakuwa kozi hiyo ni moja ya shughuli zao za kijamii wazifanyazo.

Amesema utoaji wa mafunzo hayo ya kisasa utasaidia pia kuongeza thamani yq mazao ya samaki.

“Vifaa hivi ni vya kisasa ambavyo vimegharamiwa na China hivyo ni muhimu Veta wakavitumia kwa weledi kwakuwa mafunzo hayo yamelenga kuboresha sekta hiyo,” amesema Joyce.

Amesema China wamekuwa wafadhili katika sekta mbalimbali hapa nchini ambapo kozi hiyo ya itasaidia kutoa wahitimu waliobobea na wenye weledi kwa maendeleo ya uchumi wa nchini.

Amesema vifaa hivyo vitakwenda kutumika katika chuo Cha ufundi stadi Cha Wilaya ya Chato ikiwa ni utekelezaji wa ahadi iliyotolewa na waziri Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya watu wa China, ambapo hayati Rais Dkt John Magufuli alimuomba kumsaidia vifaa katika chuo hicho.

Kwa upande wake, Balozi wa China nchini Tanzania, Dk Wange KE amesema kuwa China wamekua wakiisaidia sana Tanzania katika nyanja mbalimbali za kimaendeleo ikiwemo kutoa msaada ya vifaa pamoja na pesa kwa ajili ya kuleta Maendeleo.

Amesema kuwa wamekua wakiwasaidia wanafunzi kwenda kusoma nje kwani wao wanaamini elimu ndio uti wa mgongo, ndio maana kila mwaka tumekua tukiwasaidia wanafunzi kuwasomesha China.

Hata hivyo, amesema kuwa, anaimani sana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, hivyo China itaendelea kuisaidia Tanzania na kudumisha urafiki wao.

Naye, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), Dk Pancras Bujulu kuwa vifaa hivyo vitakwenda kusaidia katika kuhakikisha wanatoa mafunzo bora kwa wanafunzi hao.

Aidha amesema kuwa, kozi ya uchakataji samaki ni kozi ya kwanza kuanzishwa katika chuo Cha VETA , hivyo vifaa hivyo vitasaidia kuboresha mafunzo yatakayotolewa katika chuo hicho.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,307FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles