25.3 C
Dar es Salaam
Monday, July 4, 2022

VETA yajivunia kuwa na asilimia 65 ya watendaji sekta zote waliopitia kwao

DERICK MILTON-SIMIYU

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi(VETA )kanda ya magharibi Wilhard Soko amesema asilimia 65 ya watendaji wa sekta zote Nchini ni wale waliopitia elimu na mafunzo stadi kutoka katika vyuo vyao mbalimbali vya ufundi.

Sambamba na hilo VETA Imeendelea kubuni teknolojia mbalimbali za kisasa ambazo zimekuwa na mchango mkubwa katika kuleta mabadiliko katika sekta ya kilimo, viwanda, mifugo na uvuvi.

Mkurugenzi huyo amesema hayo leowakati wa mazungumzo yake na Mtanzania Digital ilipotembekea banda la maonesho la VETA lililopo viwanja vya maonesho ya nane nane vya Nyakabindi Mjini Bariadi.

Soko amesema kuwa toka kuanzishwe kwa mamlaka hiyo (VETA) wamekuwa wakijivunia mafanikio na ubunifu wa teknolojia mbalimbali za kisasa kufanya idadi kubwa ya wananchi kuamini ubunifu wa teknolojia wanazozitengeneza.

“Tunajivunia kuwa na mamlaka hii inayosimamia vyuo vyetu kwani elimu,ujuzi,ubunifu na teknolojia za kisasa zinazotolewa zinadhihirisha kuwa tuko vizuri na tunazidi kuzalisha wataalam wengi zaidi ambao wengi wao ndio hao wanaofanya kazi katika taasisi mbalimbali Nchini” amesema.

” na vitu vyote na teknolojia tunazozibuni tunaviongezea thamani siku hadi siku kwa kuzingatia sekta muhimu za kilimo,mifugo na uvuvi” amesema Soko

Ameeleza kuwa kwa sasa ile dhana potofu ya wananchi juu ya mafunzo yanayotolewa na VETA kuwa ni ya wale waliofeli elimu ya msingi na sekondari imeondoka kwani kwa sasa ujuzi wa vitendo ndio unaohitajika katika sekta mbalimbali.

” kazi za ubunifu na ufundi wa mikono kamwe haziwezi kuwa za watu walioshindwa na hii inajidhihirisha wazi kwa wahitimu wetu wa VETA ambao kwa sasa ndio wajuzi na wabunifu wa teknolojia za kisasa Nchini” amesema.

Aidha Soko ametoa wito kwa wananchi na vijana kuamini ubunifu na teknolojia zinazotengenezwa na wataalam kutoka vyuo vyao huku akiwataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika banda lao la maonesho lililopo katika viwanja vya Nyakabindi kwa ajili ya kujionea na kujifunza teknolojia mpya za Kilimo,viwanda ,uvuvi na ufugaji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
195,649FollowersFollow
545,000SubscribersSubscribe

Latest Articles