27.3 C
Dar es Salaam
Thursday, November 14, 2024

Contact us: [email protected]

Veta Tabora wanadi kozi ya useketaji Maonesho ya Nanenane

Na Nora Damian, Mtanzania Digital Dodoma

Chuo cha Ufundi Stadi Veta Tabora kimewahamasisha vijana kwenda chuoni hapo kupata mafunzo ya Useketaji ambayo yanatolewa na chuo hicho pekee.

Akizungumza Agosti 4,2024 Mwalimu wa Useketaji kutoka Chuo cha Veta Tabora, Diana John, amesema mafunzo hayo yanamwezesha kijana kujiajiri na kujiongezea kipato kwa kuzalisha bidhaa mbalimbali.

Mwalimu huyo alikuwa akizungumza kwenye Maonesho ya Wakulima na Wafugaji Nanenane yanayofanyika kitaifa jijini Dodoma ambapo pia wanaonesha bidhaa mbalimbali za useketaji.

“Ujuzi wa Useketaji unapatikana Veta Tabora tunatengeneza vitambaa vya aina mbalimbali, vikoi, mashuka, ‘bed cover’ na ‘table max’.

“Tunapokea wanafunzi wa aina mbalimbali, tuna mashine za aina mbili; mashine ya mezani na mashine ya kuweka chini. Mashine ya mezani ni kwa mtu yeyote hata kama ni mzee anachukua anaiweka mezani na kuanza kutengeneza vitambaa vidogo vidogo.

“Mashine hii ina uwezo wa kutengeneza vitu vya aina mbalimbali, tunatengeneza kwa kutumia kutumia nyuzi ambazo zimetengenezwa kwa pamba za hapa hapa Tanzania. Kwahiyo tuleteeni watoto ili waweze kupata ujuzi wa useketaji,” amesema Mwalimu Diana.

Mwalimu huyo amesema mwitikio wa wanafunzi kwenye kozi hiyo si mkubwa kutokana na ajira zake hazipatikani kwa wingi.

“Wazazi walenge watoto kujitegemea na wasifikirie kuajiriwa kwa sababu hii fani kwa mzazi mwenye malengo anaweza kumleta kijana wake au yeye mwenyewe akasoma kozi fupi na akatengeneza fedha nyingi,” amesema.

Hata hivyo amesema kama viwanda vya nguo vikifufuliwa itakuwa rahisi kuwaajiri vijana wa Kitanzania na kuweza kuzalisha bidhaa mbalimbali za nguo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles