VETA: Sasa malighafi kupatikana ndani na nje ya nchi

0
794

Asha Bani – Da re salaam

Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), Peter Maduki, amesema kwa sasa malighafi zitaweza kupatikana ndani na nje ya nchi kutokana na ubunifu mkubwa uliopo.

Ametoa kauli hiyo leo Jumamosi Julai 6, katika viwanja vya Saba saba kwenye maonesho ya Biashara ya Kimataifa.

Amesema VETA wanatakiwa kufika mpaka vijijini ambapo kuna watumiaji wa vifaa mbalimbali ikiwemo mashine ya kubungulia mahindi iliyotengenezwa na mamlaka hiyo.

Aidha amesema VETA wanashirikiana na Shirika la kuendeleza Viwanda vidogo vidogo (SIDO) pamoja na Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) ili kuweza kufikia lengo la uchumi wa viwanda waliojiwekea watanzania kwa kushirikiana na Serikali.

“Kwa sasa VETA inafanya vizuri kwa kushirikiana ba wadau husika wakiwemo taasisi zinazotoa mikopo midogo midogo kwa ajili ya kuwapa mitaji wanafunzi wanaohotimu,kutoa masomo ya ujasiriamali ,tumeingia mkataba na Sido, na taasisi mbalimbali za kifedha,”alisena Maduki.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here