Venezuela yaifungia Brazil

0
879

CARACAS, VENEZUELA

RAIS wa Venezuela, Nicolas Maduro, ameamuru kufungwa kwa mpaka wa Kusini mwa nchi yake, ambao unaitenganisha na Brazil, hatua ambayo imeanza kutumika juzi ikiwa ni ishara ya kuvunjika kwa mahusiano ya kidiplomasia baina ya mataifa hayo ya Amerika Kusini.

Uamuzi huo umechukuliwa kutokana na kile rais wa Venezuela, amekiita uchokozi kutoka Serikali ya mrengo wa kulia ya Brazil na ambao hauvumiliki.

Maduro amesema pia Venezuela inafuatilia kwa karibu hali kwenye mpaka wake na Colombia kabla ya kuchukua maamuzi yoyote.

“Sitaki kuchukuwa aina hiyo ya maamuzi, lakini ninajifunza uwezekano wa kuchukuwa hatua kama hiyo, kufunga mpaka wa Venezuela na Colombia,” amesema Maduro.

Colombia na Brazil wamejiunga na upinzani wa mrengo wa kulia nchini Venezuela kwa msimamo wao mmoja wa kumtimua rais Maduro na chama cha Kisoshalisti cha PSUV.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here