22.9 C
Dar es Salaam
Sunday, June 23, 2024

Contact us: [email protected]

Vazi litakalovaliwa na wengi ndilo la Taifa

Profesa Hermans MwansokoNA MWANDISHI WETU

SERIKALI imezitaka jamii ziwe huru kubuni na kuanza kutumia vazi watakalochagua na mavazi yatakayoshika kasi, kupendwa na kuvaliwa na wengi yataweza kutambuliwa kuwa ndiyo vazi la utambulisho wa Mtanzania.

Mkurugenzi wa Idara ya Utamaduni, Profesa Hermas Mwansoko, alisema utambulisho wa kutumia vazi la Taifa ni jambo jema, japo utekelezaji wake ni mgumu kwa Taifa kama Tanzania lenye jamii ya makabila zaidi ya 120, pia
kuna tofauti ya hali ya hewa na mazingira, jambo linalosababisha kuwa na mavazi yanayotofautiana.

Profesa Mwansoko aliongeza kwamba wananchi wana fursa ya kuamua wenyewe aina ya mavazi yaliyopendekezwa na kamati maalumu ya vazi la Taifa ambao ni mchoro wa kitambaa cha kitenge na kanga.

Pia serikali imetoa wito kwa wenye viwanda vya nguo nchini kutengeneza vitenge na kanga za michoro iliyopendekezwa ili wananchi watakaovipenda waanze kuvishona na kuvaa.

Profesa Mwansoko alisema uamuzi wa mshono mahususi kwa kila anayependa kushona aina yake umeonekana kuinyima fursa jamii, ndiyo maana serikali imeamua kutoa uhuru kwa wananchi kujiamulia vazi la Taifa ambalo watapendezwa nalo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles