26.2 C
Dar es Salaam
Sunday, April 2, 2023

Contact us: [email protected]

Varane kuikosa michuano ya Euro

Raphael VaranePARIS, UFARANSA

BEKI wa timu ya Taifa ya Ufaransa, Raphael Varane, ameachwa kwenye kikosi cha timu hiyo kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya nyama za paja.

Varane hajajumuishwa kwenye kikosi hicho kitachoshiriki michuano ya Euro huku Ufaransa wakiwa wenyeji wa michuano hiyo.

Nyota huyo wa klabu ya soka ya Real Madrid ataukosa mchezo wa fainali ya kombe la Klabu bingwa Ulaya ambao utapigwa kesho kutwa dhidi ya Atletico Madrid.

Varane amekuwa na mchango mkubwa katika kikosi cha klabu ya Madrid katika safu ya ulinzi, hivyo alijitengenezea mazingira mazuri ya kulitumikia Taifa lake.

Mchezaji huyu atakua nje ya uwanja kwa muda wa wiki tatu mpaka nne na nafasi yake kwenye kikosi cha timu ya Taifa imechukuliwa na beki Adil Rami, mwenye umri wa miaka 30 anayeichezea timu ya Sevilla ya nchini Hispania.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,407FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles