29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, February 8, 2023

Contact us: [email protected]

Vanessa Mdee ampigia hesabu Trey Songs

vanessaNa FESTO POLEA, DAR ES SALAAM

MSANII bora wa kike Afrika Mashariki, Vanessa Mdee, ameibuka na kudai kwamba hesabu zake kwa sasa ni kwa mwanamuziki wa Marekani, Trey Songs, ambaye amewahi kushinda tuzo mbalimbali za muziki.

Vanessa kwa sasa yupo katika maandalizi ya kushiriki katika tuzo ya Loeries itakayotolewa nchini Afrika Kusini kutokana na video bora ya wimbo wa ‘Niroge’ kupata umaarufu na kupendwa na wengi.

Vanessa atakutana na Trey Songs katika wimbo wa pamoja wakati wa msimu mpya wa Coke Studio Afrika International Week ambapo ataimba wimbo wa ushirikiano na Patoranking na Trey Songs. Wasanii wengine atakaoshirikiana nao ni Stonebwoy wa Ghana na Yemi Alade wa Nigeria.

“Katika harakati zangu za kutafuta ushindi wa tuzo mbalimbali ikiwemo hiyo ninayoshindanishwa nayo nchini Afrika Kusini huwa napata nguvu kufanyakazi kwa karibu na msanii, Trey Songs, kwa kuwa naye ameshinda tuzo mbalimbali,” alieleza Vanessa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,871FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles