27.4 C
Dar es Salaam
Wednesday, August 17, 2022

Uzururaji watoto unachochea ukatili wa kijinsia

Upendo Mosha -Mwanga

VITENDO vya uzururaji wa watoto mitaani hususani katika maeneo ya vijiji, vimetajwa kuwa kichocheo kikubwa cha kuendelea kushamiri kwa matukio ya ukatili wa kijinsia licha ya Serikali kuendeleza kupambana nayo.

Mwalimu mkuu wa shule ya Orlando, iliyopo Usangi wilayani Mwanga, mkoani Kilimanjaro, Christina Mbithe, aliyasema hayo kana katika mahafali ya pili ya wanafunzi wa awali, ambapo alisema jamii na wazazi wenyewe ndio wamekuwa chanzo kikubwa cha kusababisha matukio ya unyanyasaji wa kijinsia kuendeleza.

“Pamoja na Serikali kuendelea kupambana na matukio haya bado limekuwa na changamoto kubwa kwasababu jamii bado haijataka kubadilika kwani uzururaji wa watoto mitaani haswa vijiji bado upo na umekuwa ukichangia ubakaji na ulawiti wa watoto”alisema

Alisema ni vema jamii ikaona  umuhimu wa elimu hususan kwa watoto wenye umri mdogo na kuwawahisha mashukeni badala ya kuwaacha nyumbanihatua ambayo itaepusha na vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Alisema watoto wanaobaki nyumbani wakati wana umri wa kwenda shule wanayo hatari kubwa ya kufanyiwa vitendo vya ukatili kutokana na kutokuwa na uelewa wowote wa kuweza kujitambua sanjari na uangalizi mdogo kutoka kwa jamii.

Kwa upande wake mkurugenzi wa shule hiyo, Marry Shirima alisema alihamua kufungua shule hiyo kijijini ikiwa ni kurudisha fadhila eneo alilokulia na kutoa wigo mpana kwa jamii kunufaika na elimu kupitia watoto wao.

”Nimekuwa mdau mkubwa katika sekta ya elimu na ndio maana nikaona ni vyema jamii yangu nayo iweze kunufaika kama ambavyo sehemu nyingine ikiwemo Tanga na Dar es salaam wanapata kupitia shule zangu nyingine”alisema

Alisema kutokana na fursa hiyo jamii inatakiwa kuamka na kuona umuhimu wa uwepo wa shule hiyo ili lengo la uanzishwaji wake liweze kutimia ikiwa ni sehemu mojawapo ya kuunga mkono serikali kwa kujenga misingi bora ya wataalamu wa hapo baadae.

Mkuu wa chuo cha mafunzo ya biblia Usangi mchungaji  Eliraha Mmweri,aliwataka Wazazi na walezi nchini  kuwekeza kwa watoto kwa kuwapatia elimu iliyo bora ili waweze kunufaika na fursa mbalimbali zilizopo nchini ambazo kwa kiasi kikubwa zinahitaji elimu inayokwenda sambamba na mabadiliko ya sayansi na teknolojia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,903FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles