28.6 C
Dar es Salaam
Monday, December 9, 2024

Contact us: [email protected]

UWT kusimamia wanawake uchaguzi serikali za mitaa

Derick Milton, Simiyu

Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake CCM Taifa Gaudensia Kabaka amesema kuwa umoja huo utahakikisha unawasimamia hadi wanashinda wanawake wote ambao watajitokeza kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu kupitia chama hicho.

Kabaka amewataka wanawake wale wote ambao wanajisikia kugombea kwenye uchaguzi huo unaotarajia kufanyika Novemba 24, mwaka huu, kujitokeza kwa wingi kwani uwezo na nguvu wanazo za kuweza kufanya hivyo.

Mwenyekiti huyo ametoa kauli hiyo leo wakati wa kongamano la wanawake katika Wilaya ya Busega Mkoani Simiyu lililoandaliwa na Mkuu wa Wilaya hiyo Tano Mwera na kushirikisha zaidi ya wanawake 1000.

“ Nitoe wito kwa wanawake wa hapa Busega na taifa kwa ujumla, UWT tumesema kuwa mwanamke ambaye atagombea nafasi ya uongozi yeyote kwenye uchaguzi huo kupitia CCM tutamsimamia na kuhakikisha anashinda, hivyo jitokezeni kwa wingi,” alisema Kabaka.

Katika kongamano hilo lililokuwa na kauli mbiu ya wanawake katika fursa za uchumi na uongozi, tujitokeze kwa wingi kugombea nafasi za uongozi katika uchaguzi serikali za mitaa, mada mbalimbali zilitolewa zikiwemo za ujaslimali pamoja na elimu ya kupambana na ukatili wa kijinsia.

Mkuu wa Wilaya hiyo Tano Mwera alisema kuwa wanawake hao waliamua kukusanyika kwenye Wilaya hiyo kwa ajili ya kumpongeza Rais Magufuli kwa ujenzi wa hospitali ya Wilaya na vituo vya Afya ambavyo vimeboresha huduma za afya kwenye Wilaya hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles