23.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

UWEKEZAJI SEKTA YA VIWANDA KUPUNGUZA AJIRA NCHINI

 

Na JANETH MUSHI

 

-ARUSHA

Serikali imesema uwekezaji wa mifuko ya Hifadhi za Jamii nchini katika sekta ya viwanda, utasaidia kupunguza tatizo la ajira na kuweka ushindani katika soko na kushusha makali ya bei za bidhaa zitakazozalishwa nchini.

Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Sera, Vijana na Wenye Ulemavu, Jenister Mhagama amesema hayo leo wakati akifungua mkutano wa saba wa wadau wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), mkoani Arusha na kuongeza kuwa jukumu la kukuza uchumi wa viwanda ni jukumu la wadau wote.

Amesema mifuko ya hifadhi ya jamii nchini inatarajia kuwekeza katika viwanda 27 ambavyo vitaongeza ajira zaidi ya 300,000.

“Uwekezaji huu wa viwanda unaotekelezwa na mifuko ya hifadhi ya jamii hautaathiri fedha za wanachama, hivyo nawatoa hofu wanachama na wadau kwa ujumla kuwa fedha ziko salama, viwanda vitasaidia kuongeza ajira,” amesema.

Waziri Mhagama pamoja na mambo mengine ameiagiza mifuko ya hifadhi ya jamii kuhakikisha kuwa inawafikia Watanzania wengi ikiwa ni pamoja na kuanzisha mifuko mipya ya hiari ambayo inaendana na mazingira halisi ya kitanzania.

Aidha, amesema katika mifuko yote ya hifadhi ya jamii kuna wanachama zaidi ya milioni 2.4, hivyo sekta hiyo inapaswa kuboreshwa zaidi ili kuhakikisha Watanzania wananufaika na huduma zinazotolewa na mifuko hiyo.

Kuhusu mchakato wa Serikali kuunganisha mifuko yote ya hifadhi ya jamii amesema mchakato huo ukikamilika Serikali itahakikisha sekta hiyo inakuwa endelevu na fedha za wanachama ikiwamo za mafao hazitaathirika.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles