26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Uwekezaji dhamana za Serikali waongezeka

Mwandishi Wetu -Arusha

MENEJA wa Usimamizi wa Usimamizi wa Maduka ya kubadilishia Fedha za Kigeni Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Lameck Kakulu, amesema kuwa  kwa kipindi cha kuanzia Juni hadi Desemba 2019, BoT imeshuhudia kuongezeka kwa uwekezaji kwenye minada ya  dhamana za Serikali.

Hayo aliyasema jijini Arusha hivi karibuni katika mafunzo kwa waandishi wa habari za fedha na uchumi.

Alisema kuna ongezeko la asilimia 103 ukilinganisha na kiwango ambacho Serikali ilipanga kukikopa katika kipindi hiki cha nusu ya mwaka.

Kakulu alisema hatua hiyo inakwenda sambamba na kupungua kwa riba, hasa za dhamana za Serikali ambapo zimepungua kutoka asilimia 8.5 hadi tano kwa kipindi kama hicho mwaka 2018/19.

Alisema kuwa kwa upande wa washiriki, mabenki yameendelea  kuongezeka kwenye kushiriki kutoka asilimia 67 huku mifuko ya pensheni ushiriki wao katika minada ukipanda kutoka asilimia nane hadi 20.

Kakulu alisema kwa upande wa wawekezaji binafsi, mwitikio umepanda kutoka asilimia mbili hadi 6, lakini hata hivyo uko chini na BoT ingependa uongezeke zaidi.

“Ongezeko hili linatokana na jitihada za Benki Kuu na Wizara ya Fedha kufanya uhamasishaji na kuwapa uelewa wadau wa shughuli za kiuchumi, kwamba ukiwekeza kwenye dhamana za Serikali huwezi kupoteza fedha zako ulizowekeza.

“Kipato ni kikubwa kwa sababu riba zinazotolewa kwenye hizi dhamana za Serikali ni kubwa na unao uwezo wa kuziuza kwenye soko la upili na pia unaweza kuzitumia kama dhamana katika taasisi zingine za fedha ili kukopa,” alisema Kakulu.

Alisema kuwa ili kuongeza ushiriki wa wawekezaji wadogo, BoT imeendelea na jitihada kwa kushirikiana na Soho la Hisa Dar es Salaam na Wizara ya Fedha kuhakikisha kwamba inaendeleza jukwaa ambalo litasaidia wawekezaji wadogo kushiriki kikamilifu katika minada ya dhamana za Serikali ambayo inaweza kukamilika mwakani.

“Wawekezaji wadogo wataweza kushiriki kwenye minada kwa kutumia simu na kwa kiwango kidogo cha fedha, kwa sababu kiwango cha sasa cha Sh 500 bado kinaonekana ni kikubwa na tunadhani hilo litaongeza kwa kiasi kikubwa wawekezaji wadogo kushiriki katika shughuli za uchumi wa nchi na kuongeza pato la Serikali,” alisema Kakulu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles