24.6 C
Dar es Salaam
Saturday, September 7, 2024

Contact us: [email protected]

Uwanja wa ndege Mugumu wadaiwa Mil 800/-

Na Malima Lubasha – Serengeti

 UWANJA wa ndege wa Mugumu, Wilaya ya Serengeti mkoani Mara ambao Waziri wa Malisili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla amesema utajengwa ili kufungua njia ya utalii maeneo ya kaskazini na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, unadaiwa malimbikizo ya kodi zaidi ya Sh milioni 800.

Deni hilo limebainika katika Kijiji cha Robanda, wakati wa hafla ya kutambulisha  tuzo iliyopata Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kwa kuwa hifadhi bora Afrika.

Ilielezwa deni hilo, linatokana na kodi ya ardhi ya Sh milioni 500 na riba Sh milioni 300 tangu mwaka 2006 ambapo ulikuwa ujengwe kwa ubia kati ya Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti na Kampuni ya ya Grumeti Reserves Ltd.

Dk. Kigwangalla alisema kuna changamoto za kukuza na kuendeleza utalii eneo hili, wanategemea kujenga viwanja vya ndege vya Mugumu na Simiyu ili kufungua milango ya utalii.

Alisema hadi sasa shughuli zilizoshafanyika, ni usanifu wa mradi,uthaminishaji wa eneo na kutoa fidia ya Sh milioni 400, kibali cha tathmini ya athari za mazingira na kijamii  ikiwa ni pamoja na kibali cha ujenzi wa uwanja wa ndege wa hadhi ya kimataifa.

Mwaka 2006, Grumeti Game Reserves ilitoa Sh milioni 400 kwa ajili ya kulipa fidia wananchi waliokuwa wanaishi eneo hilo na kuhamisha Shule ya Msingi Burunga.

Kwa nyakati tofauti Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Serengeti, Juma Hamsini, alisema deni hilo ilinazidi kuongezeka kwa tangu Desemba, mwaka jana wakati wa kikao cha ALAT. Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Mara, ilikuwa inadai Sh milioni 700.

Mkuu wa Wilaya hiyo, Nurdin Babu, aliitaka Wizara ya Maliasili na Utalii kulichukulia kwa uzito wake jambo hili ili wageni wa ndani na nje waweze kutua hapo hapo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles