29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, February 8, 2023

Contact us: [email protected]

Uwanja wa kisasa kujengwa Dodoma

rais-dk-john-magufuli1Na JOSEPH LINO-DAR ES SALAAM

NCHI ya Morocco imekubali kujenga uwanja mpya wa kisasa wa mpira wa miguu mjini Dodoma, utakaogharimu kiasi cha Dola za Marekani milioni 80 hadi 100.

Uwanja huo wa kisasa utakuwa mkubwa zaidi ukilinganishwa na Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, uliojengwa kwa Dola za Marekani milioni 56, ukiwa na uwezo wa kuingiza watazamaji 60,000.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli, alitangaza kujengwa kwa uwanja mpya wa mpira baada kumwomba Mfalme Mohammed VI wa Morocco ambaye yupo nchini akiendelea na ziara ya kidiplomasia na kukuza uchumi.

“Nimemwomba atajenga uwanja wa mpira wa miguu Makao Makuu Dodoma ambao utagharimu Dola za Marekani milioni 80 hadi 100 na tayari ameshakubali kutujengea,” alisema Magufuli.

Ziara hiyo imejikita zaidi katika kukuza ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara ambapo ujio wa mfalme huyo umeambatana na wafanyabiashara 150 kutoka Morocco, ambao wanakutana na wafanyabiashara wa hapa nchini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,871FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles