23.7 C
Dar es Salaam
Thursday, September 28, 2023

Contact us: [email protected]

Uwanja wa gofu kujengwa Serengeti

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

MKUU wa Majeshi Mstaafu ambaye ni muasisi wa Klabu ya Gofu ya Lugalo, Jenerali George Waitara, amesema juhudi zinafanyika ili kujenga uwanja wa gofu kwenye hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

Jenerali Waitara ametoa kauli hiyo jana Januari 29,2022 wakati wa hafla ya utoaji zawadi kwa washindi wa shindano la Johnnie Walker Waitara Trophy, iliyofanyika kwenye viwanja vya Gofu ya Lugalo, jijini Dar es Salaam.

Amesema ili kukuza mchezo wa gofu nchini inahitajika kujengwa viwanja katika maeneo mbalimbali na tayari ameshauri kujenga uwanja wa gofu katika hifadhi ya Serengeti.

Mkuu wa Majeshi Mstaafu ambaye ni muasisi wa Klabu ya Gofu ya Lugalo, Jenerali George Waitara, akizungumza katika hafla ya utoaji zawadi kwa washindi wa shindano la gofu la Johnnie Walker Waitara Trophy jana.

Aidha Jenerali Waitara ameupongeza uongozi wa Gofu Lugalo kutokana na kuimarika kwa mashindano ya Waitara Trophy ambayo kwa sasa yanashirikisha karibia klabu zote nchini.

“Mashindano kila mwaka naona yanazidi kuimarika, nashukuru sana, ni mashindano ya ndani ya klabu lakini yanapendwa na vilabu vyote,” ameeleza.

Kwa upande wake mgeni rasmi wa hafla hiyo, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Damas Ndumbaro, amesema katika jitihada za kukuza utalii wameongeza mchezo wa gofu kwenye vivutio vya utalii.

Mabingwa wa Johnnie Walker Waitara Trophy wakiwa katika picha ya pamoja na wageni waalikwa na viongoz wa gofu.

“Tulishazindua rasmi utalii wa gofu Tanzania m tangu mwezi wa tisa mwaka jana. Gofu ni maisha ya kila siku,” amesema Dk. Ndumbaro.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Klabu ya Gofu Lugalo, Brigedia Jenerali Mstaafu Michael Luwongo, amesema lengo la kufanya mashindano hayo kila mwaka ni kuendeleza kumbukumbu ya klabu hiyo kwa vizazi vijavyo.

Mwenyekiti wa Klabu ya Gofu Lugalo, Brigedia Jenerali Mstaafu Michael Luwongo.

Mshindi wa jumla katika michuano hiyo ni Joseph Tango. Mashindano yameshirikisha wachezaji wa kulipwa na ridhaa kwa madaraja A,B,C, wazee na wanawake kutoka klabu mbalimbali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,745FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles