26.3 C
Dar es Salaam
Saturday, March 30, 2024

Contact us: [email protected]

UVCCM YAWAONYA WATENDAJI WAKE

Shaka Hamdu Shaka
Shaka Hamdu Shaka

NA MWANDISHI WETU-DODOMA

UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) umewaelekeza  makatibu wake ngazi za wilaya kuacha tabia ya kupokea maelekezo ya kiutendaji kutoka Makao Makuu bila ya kuwajulisha na kuwafahamisha kimaandishi wenyeviti wa jumuiya katika wilaya zao.

Pia Umoja huo umesisitiza kuwa kila mtendaji anatakiwa kutambua  kinachohitajika katika shughuli za utendaji katika jumuiya hiyo, ni ukamilishaji wa malengo, mikakati,  mipango, ubunifu na utekelezaji wa kanuni na miongozo.

Hayo yameelezwa juzi na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa, Shaka Hamdu Shaka, wakati akizungumza na   watendaji wa wilaya pamoja na wenyeviti wa wilaya zote za Mkoa wa Dodoma wa umoja huo katika mkutano wa  kupanga na kujiandaa na namna ya Vijana wa CCM watakavyofanikisha  sherehe za miaka 40 ya kuzaliwa kwa CCM.

Shaka alisema hakuna haja kwa Katibu kumficha jambo lolote mwenyekiti wake au mwenyekiti naye akatumia mamlaka aliyonayo kuchuana na katibu wake bila sababu za msingi.

“Hakuna usiri wala kificho katika kazi zetu, katibu hana atakalotenda na kufanikiwa ikiwa atabagua watu anaofanya nao kazi, maandalizi ya mipango yake, mikakati au malengo alionayo atayaona yakikwama,” alisema Shaka.

Kaimu Katibu Mkuu huyo alisema sababu za kuitisha kikao cha makatibu na wenyeviti wa wilaya za Mkoa wa Dodoma pamoja na mambo mengine, ujumbe wake kupitia kikao hicho anataka ufike moja kwa moja wilaya nyingine nchini kwa wanajumuiya wote.

“Nazungumza na wenyeviti wetu mkiwa pamoja na makatibu katika kikao kimoja, kuanzia sasa ningependa kuona mnashirikiana zaidi ili kufanikisha dhamira na madhumuni ya jumuiya yetu na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa ujumla, sipendi mgombane wala kuvutana,” alisema Katibu huyo.

Hata hivyo, alisema utekekezaji wa majukumu ya kila siku katika utendaji lazima yatokane na kuwapo kwa mahusiano na mafahamiano bila kiongozi mmoja kujigeuza haambiliki au ndiye mwenye mamlaka ya jumuiya kuliko wenzake.

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles