UVCCM yatoa angalizo kwa wapinzani wanaotoa vitisho

0
498

Mwandishi wetu,

Wakati zoezi la kuchukua fomu kwa wanaotarajiwa kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi wa serikali za mitaa linaendelea Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) umejitokeza na kusema wanazo taarifa za uhakika kuwa maeneo mengi ambayo upinzani hauna uhakika wa kupata watu wakugombea kupitia vyama vyao wameanza kutoa vitisho na kujenga hofu kwenye jamii.

Kupitia kwa Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Tanzania Bara na mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM Taifa (NEC), Galila Wabanh’u umewataka wanachama wote wa chama hicho, viongozi na wagombea wote wanaokiwakilisha katika uchaguzi wa serikali za mitaa kutokuwa na hofu wala wasiwasi kwani wamejipanga vizuri na hakuna mtu wa kuwatisha.

“Tunatoa angalizo kwa yeyote anayepanga, anayepangwa, atakayepanga au anayetaraji kupanga au kupangwa kutekeleza mkakati wowote ovu dhidi ya CCM, amani ya nchi yetu na usalama wa wananchi kuwa hatafanikiwa kwani vijana tumejiandaa na tumeamua kwa kuzingatia sheria, taratibu na kanuni za uchaguzi pamoja na misingi ya demokrasia uchaguzi huu unamalizika kwa amani na CCM inapata ushindi wa heshima,” amesema Wabanh’u.

Aidha amewaomba watanzania waendelee kuitunza amani na kujiepusha na vitendo vya ukiukwaji wa sheria katika kipindi hiki cha uchaguzi wa serikali za mitaa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here