22 C
Dar es Salaam
Friday, August 12, 2022

UVCCM yataka Maalim Seif apewe onyo

Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad
Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad

Na Mwandishi Wetu-DAR ES SALAAM

UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), umeitaka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) iache kumchekea na kumfumbia macho Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad na badala yake imwonye ili aache kuiyumbisha nchi.

Pamoja na hali hiyo umoja huo pia umetaka kiongozi huyo achukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria ikiwemo kufikishwa mahakamani kutokana na kauli zake za chuki anazozitoa kupitia nyumba za ibada.

Akizungumza na vijana 75 wa umoja huo jana jijini Dar es Salaam, Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamdu Shaka, alisema kitendo kilichofanywa na Maalim Seif kuanza kuyatumia majukwaa ya dini akitoa mahubiri ya kisiasa ni kwenda kinyume cha Sheria ya Vyama vya Siasa  Namba 5 ya mwaka 1992.

Alisema Oktoba 7, mwaka huu, Maalim Seif baada ya kumalizika swala ya Ijumaa alitoa maneno makali ya kisiasa ndani ya Msikiti wa Mwembetanga Wilaya  ya Mjini Kisiwani Unguja ambapo alidai hatua ya uwepo wa watu kutoka bara kwenda visiwani humo kwa ajili ya kupiga kura ya maoni ya Katiba mpya.

Alisema kiongozi huyo alikwepa kuzungumzia mvutano na mgogoro wa kisiasa unaofukuta ndani ya CUF akidai suala hilo lipo mahakamani.

“Tunaitaka SMZ isimfumbie macho, tunaliomba Jeshi la Polisi kumchukulia hatua Katibu Mkuu wa CUF bila kumuonea soni, kuendelea kumvumilia au kumpuuza kunaweza kuhatarisha amani ya nchi,” alisema Shaka.

Alisema Maalim Seif anachokifanya sasa ni kutafuta huruma za kisiasa kwa kuzitumia nyumba za ibada akiukwepa uwanja wa kisiasa ili kujenga hoja  kama  wanavyofanya wanasiasa wengine.

Shaka alimtaka Maalim Seif  kama siasa zimemshinda ni busara akajipambanua kwa kuwa muhubiri wa dini ili siasa awaachie walio tayari kuheshimu sheria za nchi na maadili ya  vyama vya siasa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,504FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles