23.9 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

UVCCM wawasaka Bavicha Dodoma

Shaka Hamdu Shaka
Shaka Hamdu Shaka

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

KAIMU Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Shaka Hamdu Shaka amewasili mkoani Dodoma na kuhoji waliko vijana wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha) waliotangaza kutaka kuuvuruga Mkutano Mkuu wa chama hicho unaotarajiwa kufanyika Jumamosi wiki hii.

Shaka alisema yuko mkoani hapa kwa ajili ya kuongoza harakati za kukilinda chama hicho kwa kushirikiana na vijana wa CCM.

Alisema UVCCM imeandaa vijana 30,000 maalumu kwa ajili ya kulinda mkutano huo utakaohudhuriwa na viongozi wote wa juu wa serikali na CCM.

Kaimu Katibu Mkuu huyo alisema aliwasili mapema mkoani Dodoma ili pamoja na mambo mengine ashuhudie vurugu zilizoahidiwa na Bavicha lakini, hadi sasa hakuna chochote.

“Nipo hapa kwa muda mrefu kwa ajili ya kuongoza shughuli za ulinzi wa chama na viongozi wetu nikiwa mtendaji mkuu na mtoa maelelezo ya kiitifaki.

“Kwa bahati mbaya kwa muda wote huo sijaona dalili wala hata harufu ya Bavicha. Hii inadhihirisha kwamba kusema na kutenda ni vitu tofauti,”alisema Shaka.

Alisema azma ya UVCCM ilikuwa ni kuithibitishia dunia kwamba Watanznia hawako tayari kuona kundi lolote la wahuni likichafua amani, utulivu na usalama wa watu na likaachwa litambe  bila kufundishwa.

Shaka alisema, wajumbe wa mkutano huo hawapaswi kuwa na hofu juu ya usalama wao na mali zao na kuwaomba waingie Dodoma wakiwa na  imani na watatoka salama kwa kuwa vijana wa kuwalinda wapo wa kutosha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles