UVCCM KUWAPIGA MSASA VIJANA WAKE IHEMI

0
658

Na Mwandishi Wetu

Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) umesema umepania kukifufua na kukiendeleza Chuo cha Siasa , Uongozi na Ujasiriamali kilichopo Ihemi mkoani Iringa.

Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM,  Shaka Hamdu Shaka amesema    lengo ni kuwapika , kuwafundisha na kuwaandaa katika saikolojoa vijana ili kuwapa stadi za maisha na kujitegemea katika uchumi.

Alikuwa akizundua mafunzo elekezi ya ujasiriamali na uhamasishaji   kwa kuzitambua fursa za kujiajiri kwa  vijana wa  Wilaya ya Ubungo katika ukumbi wa Texas Manzese,   Dar es Salaam.

Shaka alisema hakuna taifa lolote duniani lenye uwezo wa kuwapatia ajira vijana wote.

Alisema  badala yake vijana huwezeshwa katika elimu kwa kufundishwa stadi za maisha, ufanyaji bora wa biashara, uendeshaji miradi , kutambua na kuzingatia vyema miiko ya chama, siasa yake na itikadi.

Alisema njia pekee ya kumuunga mkono Rais Dk. John Magufuli na kuinua maisha ya vijana dhidi ya umasikini na matumizi bora ya maliaasili na rasilimali za taifa ni vijana wenyewe kujitambua, kujituma na kujitegemea.

“Ili vijana waendesha miradi yao ya uchumi na kuwapa manufaa, biashara na kujitegemea wanahitaji kujengwa uwezo, kupewa mbinu za kisasa na kufundishwa stadi za maisha kwa weledi na umakini,”alisema Shaka.

Alisema chuo hicho sasa licha ya kutumika kuwafundisha ujasiriamali vile vile kitafundisha siasa ya chama, itikadi, na uzalendo ikiwamo kuwaeleimisha katika masuala ya kujitegemea na ufundi.

Akizumgumzia maendeleo ya uchaguzi ndani ya chama na jumuiya zake,   aliwataka watendaji wa jumuia kusimaia miongozo na kanuni huku wagombea wakitakiwa kutojihusisha na vitendo vya rushwa.

Alisema uchaguzi ni lazima utoe viongozi wenye uthubutu, uwezo wa kuitetea jumuiya, kuipigania na kuweka katika taaswira ya kuheshimika jambo litakalosaidia kuwapata viongozi  bora, makini, wenye ujasiri na uzalendo.

“Nasema tena hakuna mgombea atakayepitishwa na vikao vyetu ikiwa sifa zake zina kasoro, upungufu au zwa kuokotezaokoteza.

“Tutampekua kila mgombea na tukimuona hatokani na CCM tutamtosa bila ya kuutazama uso wake,” alisistiza.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here