UVCCM Kilimanjaro kuchangia damu majeruhi ajali lori la mafuta

0
703

Safina Sarwatt, Moshi

Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Kilimanjaro wanatarajia kufanya shughuli ya uchangiaji damu kwa ajili majeruhi waliopata ajali ya moto iliyotokea mkoani Morogoro Agosti 10 mwaka huu, baada ya lori la mafuta kupinduka na kulipuka na kusababisha vifo vya watu 89.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Moshi leo Ijumaa Agosti 16, Katibu wa UVCCM Mkoa wa Kilimanjaro, Asia Halamga , amesema shughuli hiyo itafanyika Agosti 17 mwaka huu katika Uwanja wa Hindu Mandal ulipo mjini hapa.

“Tunatarajia kukusanya kiasi cha uniti 70 pia tunawaomba wananchi wenye mapenzi mema kujitokeza kuchangia damu ili kuokoa maisha ya Watanzania,” amesema.

Aidha, amesema zoezi hilo la kuchangia damu halihusiani na chama chochote bali ni Watanzania wote wenye nia na upendo wa kusaidia wajitokeze kwa wingi kuungana nao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here