25.6 C
Dar es Salaam
Sunday, January 5, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

UUZWAJI HISA VODACOM WAONESHA UDHAIFU WA MIFUMO

Baadhi ya wanachama wa Muungano wa Vyama vya Ushirika (SACC OS) Tanzania , wakisoma fomu za kununua hisa za Vodacom Tanzania PLC.

 

 

Na Mwandishi Wetu-DAR ES SALAAM

PAMOJA na zaidi ya wahitaji 40,000  kuvutiwa na hisa za Vodacom Tanzania PLC na kuzilipia mamlaka  za usimamizi, zimeonesha mapungufu mengi ya usimamizi na kuweka wawekezaji roho juu kwa zaidi ya mwezi mmoja bila kujua hatima ya ununuzi huo.

Wameomba mamlaka  hizo za DSE na CMSA kuwa imara na kufanya kazi kileo na kutumia teknolojia stahiki ili kurahisisha na kukimbiza mwendo wa kushughulikia mambo zaidi ya hali ilivyo sasa ambako  kumeonesha mwendo wa kujivuta kinyume na mategemeo  ya wengi na hivyo kuwakwamisha wengi katika kupata faida ya haraka haraka kutokana na hisa hizo.

“Kila mtu ananunua hisa kwa malengo yake, wengine kwa muda mfupi na wengine kwa muda mrefu na hivyo wale wa muda mfupi waliokopa pesa ili washiriki katika zoezi hili na kupata faida ya chapuchapu wamekwama,” alilalamika mteja mmoja ambaye hakutaka kusema jina lake ambaye alinunua hisa 10,000.

Uuzaji wa hisa za Vodacom kwa muda wa ziada ulifungwa tarehe 19, Mei na hivyo kushangaa  zoezi la kuhesabu na kuwapa watu lilikuwa halijakamilika na kuendelea na mchakato wa kuingia sokoni.

Cha kushangaza hadi jana CMSA ilikuwa haijatoa kiasi cha mauzo kilichopatikana na hivyo kuleta wasiwasi kuwa huenda mambo hayakuwa mazuri na kutofikiwa lengo.

Lakini wajuzi wa mambo ya soko la hisa, wanasema ukiona kuna ukimya mwingi ni kuwa mauzo yamefana (oversubscription) na hivyo kunahitajika kazi ya ziada ya panga pangua ili kupata mgao unaoridhisha kwa washindi na hivyo mamlaka huingia kazi ya ziada na kupata ushauri ‘kwingineko’.

Toleo la Kwanza (IPO)

Hisa za Vodacom zitakuwa za kihistoria kwa mambo mengi ikiwamo asili yake na ukubwa wa toleo na kutegemewa kuvunja rekodi katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) kwa miaka 19 tangu kuanzishwa kwake.

Hiyo ni mara ya kwanza kwa kampuni kuuza hisa zake kwa lazima kwa ajili ya kufuata  mahitaji ya sheria na si kuhitaji fedha kama mtaji na hivyo inawafanya wengi kutaka kujua itakuwaje kwani mwenendo mzima ni mchecheto na mgeni.

Kama Vodacom ikishindwa kutengeneza faida kwenye soko ambalo linaonekana limejaa (saturated) kwa mambo ya simu lawama azibebe nani? Kwanini kampuni nyingine zinaendelea kuwepo sokoni  wakati hazijajiunga na soko?

Kama tukienda kwa mwenendo anaotaka Rais Magufuli, ni kuwa zifutwe na kwanini TCRA hawajatekeleza msimamo huo? Ni mbaya kwa soko kuwa na soko lenye masharti tofauti kwa washiriki wake yaani litakosa mwelekeo (level.)

Taarifa  za awali toka Vodacom zinasema zaidi ya Watanzania 40,000, wengi wao wakijitokeza kwa mara yao ya kwanza, wamenunua hisa hizo kwa ari na majigambo ya Watanzania kumiliki kampuni kubwa zinazofanya biashara nchini.

Akizungumzia hali hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC, Ian Ferrao, aliwashukuru watu binafsi na mashirika kwa uwekezaji huo kupitia kampuni hiyo na kusema kuwa huenda biashara katika hisa zake katika Soko la Hisa la Dar es Salaam inatarajiwa kuanza mwezi huu baada ya kukamilika kwa uhakiki unaofanywa na Mamlaka ya Masoko na Mitaji Tanzania (CMSA).

Akizungumza na waandishi wa habari, Ferrao aliwashukuru watu binafsi na mashirika ya uwekezaji kwa kushiriki kwao kwenye zoezi hili la kununua hisa zetu, tunatarajia kuwa na uhusiano mzuri wenye manufaa kwa washirika wetu wapya wakati tukiipeleka kampuni yetu kwenye hatua muhimu na bora zaidi na kuwa kampuni iliyoorodheshwa kwenye Soko la Hisa la Dar es Salaam.

Alitamba kuwa Vodacom Tanzania PLC inajivunia kuwa kampuni ya mawasiliano inayoongoza hapa Tanzania na ndiyo maana leo hii tumekuwa kampuni ya kwanza kutimiza masharti ya Bunge la Tanzania ya kutaka makampuni yote ya simu za mkononi kuorodhesha hisa zake kwenye Soko la Hisa la Dar es Salaam.

Alisema kutokana na wingi wa maombi ya waliojitokeza wakati wa mauzo, yalichukua muda mrefu kuliko ilivyotegemewa na maombi yalishughulikiwa kwa haraka.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles