25.6 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 1, 2021

Uuzaji kahawa nje washuka kutoka tani 25,000 hadi 5000

Na SAFINA SARWATT-MOSHI  

KATIBU mkuu Wizara Kilimo Gerald Kusaya amesema kuwa uuzwaji wa zao la kahawa kwenda nje ya nchi kwa mkoa wa Kilimanjaro umeshuka kutoka tani 25,000 hadi kufikia  5000.

Katibu mkuu huyo aliyasema hayo jana katika ziara yake ya kikazi mkoani Kilimanjaro, ambapo alitembelea bodi ya kahawa (TCB), kiwanda cha kukoboa kahawa cha TCCCo kinachomilikiwa na  chama kikuu cha ushirika mkoa wa Kilimanjaro KNCU pamoja taasisi za utafiti wa kahawa nchini TACRI. 

Alisema takwimu za uuzwaji wa kahawa nje ya nchi katika kipindi cha nyuma Mkoa wa Kilimanjaro ulikuwa unauza kahawa tani 25,000 lakini kwasasa unauza tani 5,000 za kahawa nje ya nchi.  

“Hili ni changamoto,”alisisitiza 

Alisema lengo la serikali ni kuhakikisha kupitia taasisi hizo zinazohusika na kahawa uzalishaji unaongezeka.

Alisema kuwa wizara ya kilimo imejipanga kuhakikisha inasimamia taasisi hizo kwa kuziongezea watalamu pamoja na kuzitengea fedha nyingi, ili kuboresha hali ya uzalishaji wa kahawa bora inayokubalika katika soko la dunia. 

“Kuwapatia mbengu bora yenye tija kubwa ili kuongeza uzalishaji wa zao la kahawa hapa nchini kwani lengo la serikali ni kuongeza uzalishaji wa zao Kahawa,”alisema. 

“Nimefarijika sana taasisi hii ya utafiti wa kahawa kwa jitihada kubwa zinazofanywa na watafiti, kwa  kufufua zao la kahawa kwani  lengo la 

Serikali ni kuhakikisha inafufua kahawa,”alisema. 

“Wizara imeweka mikakati ya kuhakikisha kwamba inaongeza uzalishaji wa zao la kahawa kwa kuongeza watalamu pamoja na kutenga fedha nyingi kwa ajili ya utafiti na kuzalishaji miche bora ya kahawa,”alisema. 

 Alisema erikali inapata fedha nyingi kutoka kwenye zao la kahawa ,hivyo wizara hiyo inatendelea na mikakati yake kuhakikisha zao hilo linazalishwa kwa wingi.

Akizungumzia malengo mengine alisema ni kuhakikisha kila kata kuna ofisa ugani ili kuwawezesha wakulima kupata elimu ya kutosha kuhusu uzalishaji wa kahawa. 

Akizungumza hali ya  vyama vya ushirika  nchini alisema, bado haijamfurahisha rais kutokana utendaji  mbovu wa viongozi wa vyama hivyo  na ushirika kuonekana kuwa chombo cha migogoro. 

Alisema wanataka ushirika ule ambao unafanya biashara na si wa migogoro.

“Tunatakiwa kuwa viongozi wabunifu watakaofanya miradi endelevu kwa lengo la kuimarisha ushirika na kurudisha uhai vyama vya ushirika. 

Mtafiti wa usambazaji wa teknolojia na mafunzo kutoka taasisi ya utafiti wa kahawa nchini (TaCRI), Jeremiah Magesa alisema taasisi hiyo  inashirikiana  na halmashauri 68 nchini lengo ni kuhakikisha wanakidhi mahitaji ya miche bora ya kahawa. 

Alisema mahitaji ya miche kwa sasa ni makubwa na imeweka mikakati ya kuzaliza miche milion 20 kwa mwaka ili kuhakikisha uzalishaji wa zao hilo unaongezeka. 

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,526FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles