31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Uturuki yazuia wasomi kusafiri nje ya nchi

Raisi Recep Tayyip Erdogan
Raisi Recep Tayyip Erdogan

ANKRA, UTURUKI

SERIKALI ya Uturuki imeweka kwa muda zuio kwa wasomi wote nchini hapa kusafiri nje, ikiwa ni hatua ya kuwasaka waliohusika na jaribio lililoshindwa la mapinduzi.

Zaidi ya watu 50,000 wamekamatwa, kufutwa au kusimamishwa kazi wakiwemo walimu wapatao 21,000.

Rais Recep Tayyip Erdogan alitumia muda mwingi jana kufanya vikao na maofisa wa usalama wa nchi na baraza lake la mawaziri.

Ni mara ya kwanza kufanya mkutano huo tangu jaribio la kupindua serikali yake liliposhindikana Ijumaa iliyopita.

Rais Erdogan anajaribu kurudisha utulivu, lakini pia anashutumiwa kwa kuwalenga wapinzani wake akitumia kisingizio cha jaribio hilo.

Wasimamizi wa vitivo vya vyuo vikuu wapatao 1,577 wametakiwa kujiuzulu pamoja na walimu 21,000 na maafisa wa wizara ya elimu karibu 15,000.

Mara tu baada ya jaribio hilo la mapinduzi kutibuka wengi wa wanajeshi, maafisa usalama na watumishi wa umma walikamatwa au kufutwa kazi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles