26.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 27, 2021

UTURUKI YAWAFUKUZA WANAJESHI 4,000

ISTANBUL, UTURUKI


SERIKALI ya Uturuki imewafuta kazi watumishi wa umma na wanajeshi 4,000 wanaoshukiwa kuwa tishio kwa usalama wa taifa.

Hiyo inakuwa mara ya pili kwa utawala wa Rais Recep Tayyip Erdogan kuwafuta kazi maelfu ya watu tangu aongezewe madaraka kupitia kura ya maoni iliyofanyika mwezi uliopita.

Waliofutwa kazi ni pamoja na askari wa magereza, makarani, wasomi, wafanyakazi wa taasisi za kidini na wanajeshi 1,200 wakiwemo maafisa 600.

Watu hao wanatuhumiwa kuwa na uhusiano na makundi ya kigaidi na mifumo ambayo ni tishio kwa usalama wa taifa.

Hatua hiyo ya juzi inakuja baada ya Jumatano wiki iliyopita kushuhudia maofisa 9,000 wa polisi wakisimamishwa kazi na wengine 1,000 wakihusishwa na mtandao wa mpinzani wa Erdogan, Fethullah Gulen anayeishi Marekani.

Utawala wa hapa unamshutumu kiongozi huyo wa kidini kupanga jaribio la kuipindua serikali lililoshindwa mwaka jana.

Tangu jaribio hilo watu 120,000 wamesimamishwa au kufukuzwa kazi na zaidi ya 40,000 kukamatwa.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
163,388FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles