24.1 C
Dar es Salaam
Saturday, September 23, 2023

Contact us: [email protected]

Uturuki yaua watu 35 Syria

000cc4cc-642

ISTANBUL, UTURUKI

MASHAMBULIZI ya anga yanayofanywa na jeshi la Uturuki yamesababisha vifo vya watu 20 na kujeruhi wengine jana subuhi katika kijiji cha kaskazini mwa Syria.

Shambulio lingine limetokea kusini mwa mji wa mpakani wa Jarabulus unaodhibitiwa na waasi wanaoungwa mkono na Uturuki na kusababisha vifo vya raia 15 na kujeruhi wengine 25

Katika mashambulizi hayo, Uturuki na washirika wake wa kundi la waasi wa Syria wanapambana na wanamgambo wanaoungwa mkono na Wakurdi.

Shirika la Kuteta Haki za Binadamu la Syria limesema watu 50 wamejeruhiwa katika shambulio la kijiji cha Jub al-Kousa katika eneo linalodhibitiwa na wanamgambo washirika wa Chama cha Demokrasia cha Wakurdi.

Ni siku ya tano ya kampeni ya mashambulizi ya Uturuki dhidi ya vikosi vya Kikurdi pamoja na wapiganaji wa kundi linalojiita Dola la Kiislamu (IS) nchini Syria.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,699FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles