27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, February 8, 2023

Contact us: [email protected]

UTURUKI YAPELELEZA RAIA WAKE UJERUMANI

BERLIN, UJERUMANI


SERIKALI ya Ujerumani imewatahadharisha Waturuki waishio hapa kuwa Serikali ya Uturuki inafanya upelelezi dhidi yao na kuwapiga picha kwa siri.

Vyombo vya habari vya Ujerumani viliripoti kuwa idara za ujasusi za Uturuki zinawatuhumu mamia ya raia wa nchi hiyo waishio hapa kuwa wafuasi wa muhubiri wa Kiislamu, Fethullah Gulen.

Kwa sababu hizo, mamlaka za Uturuki zimekusanya taarifa kuwahusu na kuzikabidhi kwa vyombo vya usalama vya Ujerumani.

Kwa mujibu wa gazeti la Suddeutsche Zeitung, taarifa hizo za upelelezi zina anuani, nambari za simu na picha zilizopigwa kwa siri kwa kutumia kamera za uchunguzi.  

Zaidi ya watu 300, klabu 200, shule na taasisi nyingine zinahusishwa kuwa na uhusiano na Gulen anayeishi Marekani.

Mkuu wa Idara ya Ujasusi nchini Ujerumani, inayofuatilia masuala ya nje, alikabidhiwa orodha hiyo na mwenzake wa Uturuki wakati wa mkutano wa kimataifa wa masuala ya usalama uliofanyika hapa.

Lakini baadaye Serikali ya Ujerumani iliwatahadharisha watu hao kuwa wanafuatiliwa na Uturuki.

Serikali ya Uturuki inamtuhumu Gulen kwa kuratibu jaribio la mapinduzi lililoshindwa  Julai mwaka jana.

Gulen amekuwa akikana madai hayo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,871FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles